Mashangilio 13

Mashangilio 13

Mpaka lini, Bwana?

1Mpaka lini, Bwana, utanisahau kila mara? Mpaka lini utauficha uso wako, usinione?[#Sh. 77:8; Hab. 1:2.]

2Mpaka lini nitie wasiwasi rohoni mwangu na masikitiko moyoni mwangu kila siku? Mpaka lini ataniinukia mchukivu wangu?

3Nitazame, ukaniitikie, Bwana Mungu wangu! Yaangaze macho yangu, nisipatwe na usingizi uuao!

4Mchukivu wangu asiseme: Nimemshinda! Nao wanisongao wasishangilie, ya kuwa nimetikisika!

5Nami nimeuegemea upole wako; moyo wangu hushangilia, ya kuwa unaniokoa; nitamwimbia Bwana kwa ajili ya mema, aliyonitendea.[#Sh. 9:15.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania