Mashangilio 130

Mashangilio 130

Kuomba ondoleo la makosa.

(Wimbo wa juto wa 6.)

1*Humu, nilimo vilindini, ninakulilia, Bwana.[#Sh. 69:3.]

2Ninakuomba, Bwana, uisikilize sauti yangu! Masikio yako na yaziangalie sauti za malalamiko yangu!

3Bwana, kama unazishika manza, watu walizozikora, yuko nani atakayesimama mbele yako wewe?[#Sh. 19:13.]

4Lakini kwako liko ondoleo la makosa, kusudi watu wakuogope.[#Yes. 55:7; Rom. 6:1-2.]

5Ninamngojea Bwana, nayo roho yangu inamngojea, nalo Neno lake ndilo, ninalolitazamia.

6Roho yangu inamngoja Bwana, inashinda walinzi wa usiku, ndio walinzi wa usiku wanaongoja, kuche.

7Waisiraeli na wamngoje Bwana! Kwani kwake Bwana kuna upole, nao ukombozi uko kwake wa kukomboa wengi.

8Yeye atawakomboa Waisiraeli katika manza, walizozikora zote.*[#Mat. 1:21.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania