The chat will start when you send the first message.
1Bwana, unanichunguza, unanijua.[#Sh. 7:10; 139:23.]
2Wewe unajua kukaa kwangu na kuinuka kwangu, ukayatambua mawazo yangu, ijapo uwe mbali.[#Yer. 17:10.]
3Kma ninakwenda au ninalala, unanivumbua, njia zangu zote zimekuelekea.
4Kwani hakuna neno, ulimi wangu utakalolisema, usilokwisha kulijua lote, wewe Bwana.
5Nyuma na mbele umenifungia, ukanibandikia mkono wako.
6Ni ya kustaajabu, sitaweza kuyatambua, ni mambo makuu, sitaweza kuyafumbua.
7Nihamie wapi, Roho yako isinijie? Nikimbilie wapi, uso wako usinione?
8Kama ningekwenda kupaa mbinguni, wewe uko; kama ningekwenda kulala kuzimuni, wewe uko.[#Amo. 9:2.]
9Kama ningetumia mionzi ya jua kuwa mabawa yangu, nikaja kukaa mapeoni kwenye bahari,[#Yona 1:3.]
10huko nako mkono wako ungeniongoza, mkono wako wa kuume ungenishika.
11Kama ningesema: Giza na liniguie, nao mwanga unizungukao na uwe usiku,[#Iy. 34:22.]
12giza nalo lisingekuwa lenye weusi machoni pako; maana usiku huangaza kama mchana huko uliko, kwako giza na mwanga huwa sawasawa.[#Yak. 1:17.]
13Kwani wewe ndiwe uliyeyaumba mafigo yangu, ndiwe uliyeniunga tumboni mwa mama.
14Ninakushukuru, kwani ni ajabu litishalo, jinsi nilivyotengenezwa, vilivyo kazi zako hustaajabisha kweli, roho yangu inavijua sanasana.
15Mifupa yangu haikuwa imefichika, usiione, nilipofanyiziwa mahali palipojificha, maana nilitengenezwa mbali sana ndani ya nchi.[#Mbiu. 11:5.]
16Nilipokuwa mimba tumboni mwa mama, macho yako yaliniona, nazo siku zangu zote zilikuwa zimeandikwa kitabuni mwako hapo, zilipoambiwa, zitokee; ilikuwa hapo, hata moja yao ilipokuwa haijawa bado.[#Iy. 14:5.]
17Lakini kwangu ni vigumu sana kuyajua mawazo yako, Bwana, nikiyachanganya, yako na nguvu za kunishinda.[#Yes. 55:9.]
18Yangekuwa mengi kuliko mchanga, kama ningeweza kuyahesabu. Ningaliko kwako bado ninapoamka.[#Sh. 40:6; 63:7.]
19Nakuomba, Mungu, uwaue wasiokucha, wenye manza za damu waondoke kwangu;
20ndio wanaokutaja tu, wapate kuuficha ukorofi wao; kwa kuwa wabishi wako, hujivuna bure.
21Wachukizwao na wewe, Bwana, nisiwachukie? Nao wakuinukiao nisitapishwe nao?
22Ninawachukia kwa uchukivu usiosaza hata kidogo, ninawatazama kuwa adui zangu mimi.
23Nichunguze, Mungu, uujue moyo wangu! Nijaribu, uyajue nayo mawazo, niliyo nayo![#Sh. 139:1.]
24Tazama, kama nimeshika njia iendayo kwenye maumivu, unishikishe njia iendayo kwenye kuwapo kale na kale!