Mashangilio 14

Mashangilio 14

Upumbavu wao wasiomcha Mungu.

(Taz. Sh. 53.)

1Mpumbavu husema moyoni mwake: Hakuna Mungu. Hawafai kitu, mapotovu yao hutapisha, anayefanya mema hayuko.

2Bwana huchungulia toka mbinguni awatazame wana wa watu, aone, kama yuko mwenye akili anayemtafuta Mungu.[#Sh. 33:13.]

3Wote pamoja wamepotelewa na njia, wote ni waovu, hakuna anayefanya mema; hakuna hata mmoja.[#1 Mose 6:12; Rom. 3:10-12; Tit. 1:16.]

4Je? Wale wote wafanyao maovu hawataki kujitambua, wao wanaowala walio ukoo wangu, kama walavyo mkate? Lakini Bwana hawamtambikii![#Mika 3:3.]

5Patafika, watakapotetemeka kwa kustuka, kwani Mungu yuko kwao walio wazao waongokao.

6Shauri la mnyonge mnalibezesha, kwa maana Bwana ndiye, anayemjetea.[#Sh. 12:6.]

7Laiti mwokozi wake Isiraeli atokee Sioni, Bwana awarudhishe mateka walio wa ukoo wake! Ndipo, Yakobo atakaposhangilia, ndipo, Isiraeli atakapofurahi.[#Luk. 2:25-32.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania