The chat will start when you send the first message.
1Haleluya! Mshangilie Bwana, roho yangu!
2Na nimshangilie Bwana siku zangu za kuwapo! Na nimwimbie Mungu wangu na kupiga zeze nikingali nipo!
3Msiegemee wakuu! Nao ni wana wa watu, hawawezi kuokoa.[#Sh. 118:8-9; Yer. 17:5.]
4Roho ya mtu ikimtoka, inarudi mchangani; siku ile mizungu yake itakuwa imepotea.[#1 Mose 3:19; Mbiu. 12:7.]
5Mwenye shangwe ni mtu wa Mungu wa Yakobo, maana humsaidia, akimngojea Bwana, Mungu wake.
6Yeye ndiye aliyezifanya mbingu na nchi, hata bahari navyo vyote vilivyomo. Yeye ndiye ashikaye welekevu na kuufuata kale na kale.
7Yeye ndiye anayewaamulia waliokorofishwa, yeye ndiye anayewashibisha wenye njaa.
Yeye Bwana ndiye anayewafungua waliofungwa,
8yeye Bwana ndiye anayefumbua macho ya vipofu, yeye Bwana ndiye anayewainua walioinamishwa, yeye Bwana ndiye anayewapenda waongofu,[#Sh. 145:14.]
9yeye Bwana ndiye anayewaangalia nao wageni, nao waliofiwa na wazazi, hata wajane huwaegemeza, lakini njia yao wasiomcha huipoteza.[#2 Mose 22:21-22; Sh. 10:14; 68:6.]
10Bwana anashika ufalme kale na kale, Mungu wako, Sioni, ni wa vizazi na vizazi. Haleluya![#Sh. 93:1.]