The chat will start when you send the first message.
1Heleluya! Mwimbieni Bwana wimbo mpya! Mkutano wao wamchao na umshangilie![#Sh. 96:1.]
2Waisiraeli na wamfurahie aliyewafanya! Wana wa sioni na wampigie vigelegele aliye mfalme wao![#Sh. 93:1; 100:3.]
3Na walishangilie Jina lake na kucheza ngoma! Na wamwimbie na kupiga patu pamoja na mazeze!
4Kwani Bwana anapendezwa nao wlaio ukoo wake, huwaokoa watesekao na kuwapamba vizuri.
5Wamchao na wapige shangwe kwa kupate utukufu! Na wapige vigelegele katika vilalo vyao!
6Na wamtukuze Bwana kwa makoo yao! Namo mikononi mwao na washike panga zenye makali pande mbili!
7Wajipatie malipizi kwao wamizimu, makali ya hao watu wayapatilize!
8Wawafunge wafalme wao kwa minyororo nao watukufu wao kwa mapingu ya chuma!
9Wawafanyizie zile hukumu, walizoandikiwa! Macheo kama hayo watapewa wote wamchao. Haleluya![#4 Mose 21:1-3; 1 Sam. 15.]