The chat will start when you send the first message.
1Bwana, mfalme huifurahia nguvu yako, tazama, jinsi anavyoushangilia mno wokovu wako!
2Moyo wake uyatunukiayo umempa; wala hukumnyima midomo yake iliyoyaomba.[#Sh. 20:5; 37:4.]
3Kwani umemjia na kumletea magawio mema, nacho kichwa chake umekivika kilemba kilicho dhahabu tupu.[#Sh. 132:18.]
4Alipokuomba uzima, umempa kuwapo, siku zake ziwe nyingi kale na kale.
5Utukufu, aupatao, ni mkubwa kwa hivyo, unavyomsaidia, hata marembo na mapambo umempatia.
6Maana umemweka kuwa mbaraka kale na kale, ukamchangamsha, aone furaha iliyo mbele yako.
7Kwani mfalme amwegemeaye Bwana, hatatikisika kwa upoke wake Alioko huko juu.
8Mkono wako utawapata adui zako wote, kuumeni kwako kutawapata nao wachukivu wako.
9Utawafanya kuwa kama jiko la moto, utakapowatokea, Bwana atawameza kwa makali yake, nao moto utawala.
10Vizazi vyao utaviangamiza, viishie nchini, nazo koo zao sharti zitoweke kwenye wana wa watu.[#Sh. 109:13.]
11Kwani wamekutegea vibaya, wakakuwazia yenye ujanja, lakini hawakuweza kuyafanyiza.[#Yes. 8:10.]
12Kwani utawashurutisha kuonyesha migongo, wakikimbia, maana nyugwe za pindi zako utazivuta machoni pao.[#Sh. 7:13.]
13Tukuka, Bwana, kwa nguvu zako! Nasi tuimbe na kuyakuza matendo ya uwezo wako!