The chat will start when you send the first message.
1*Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Wokovu wangu uko mbali, kwa hiyo napiga kite.[#Mat. 27:46.]
2Mungu wangu, mchana kutwa nakuita, nawe hikuniitikia; usiku nao hapana, ninaponyamaza.
3Nawe ndiwe uliye mtakatifu, unakaa na kukuzwa nao Waisiraeli.
4Wewe nidwe, waliyekutegemea baba zetu, napo walipokutegemea, ukawaopoa.
5Wewe ndiwe, waliyekulalamikia, wakaponywa, wewe ndiwe, waliyekutegemea, tena hawakupatwa na soni.[#Sh. 25:2-3.]
6Lakini mimi ni kidudu, si mtu bado, watu wakanifyoza wote na kunibeza.[#Sh. 69:8; Yes. 53:3; Mat. 27:39-44.]
7Wote wanionao hunibeua, hukuza vinywa na kutingisha vichwa, kisha husema:[#Iy. 16:4,10.]
8Umsukumie Bwana! Na amponye! Kama anapendezwa naye, na amwokoe!
9Kwani ndiwe uliyenitoa tumboni mwa mama, ukaniegemeza maziwa yake mama yangu.[#Sh. 71:6.]
10Wewe ndiwe, niliyetupiwa tangu hapo, nilipozaliwa; tangu hapo, nilipotoka tumboni mwa mama, wewe u Mungu wangu,
11Kwa kuwa masongano yako karibu, usinikalie mbali! Kwani atakayenisaidia hayuko.
12Ng'ombe waume wengi wamenizunguka, nao nyati wa Basani wakanizingazinga.
13Wakaasama vinywa vyao, wanimeze, wakawa kama simba anyafuaye na kunguruma.
14Nafanana na maji yamwagwayo, mifupa yangu imeteguka yote, moyo wangu ni kama nta iyeyukayo humu mwangu ndani.[#Luk. 22:44.]
15Nguvu yangu imekupwa, nikavunjika kama gae, nao ulimi wangu umegandamana na ufizi wangu, namo uvumbini mwa kufa ndimo, ulimonilaza.[#Yoh. 19:28.]
16Kwani walikuwako mbwa, wakanizunguka, kikosi cha wabaya kikanijia pande zote, kisha wakanitoboa maganja na nyayo.[#Yoh. 20:25-27.]
17Naweza kuihesabu mifupa yangu yote, nao wanavitazama tu na kunitumbulia macho.
18Wakajigawanyia nguo zangu, nalo vazi langu zuri wakalipigia kura.[#Yoh. 19:24.]
19Nawe, Bwana, usiwe mbali! Kwa hivyo, unavyonishupaza, piga mbio, unisaidie!*
20Iopoe roho yangu kwenye panga! Hiyo iliyo mali yangu peke yake iopoe kwenye mbwa![#Sh. 35:17.]
21Namo kinywani mwa simba niokoe, kwani nilipokuwa penye pembe za nyati, uliniitikia.
22Nitawasimulia ndugu zangu mambo ya Jina lako, nitakuimbia wewe katikati yao walio wateule.[#Sh. 9:15; Yoh. 20:17; Ebr. 2:12.]
23Ninyi mmwogopao Bwana, mkuzeni! Vizazi vyote vya Yakobo na vimtukuze! Vizazi vyote vya Isiraeli na vimwangukie!
24Kwani hakuubeza unyonge wake mnyonge, wala moyo wake hakuuchafukia, wala hakuuficha uso wake, asimwone, ila alimsikia, alipomlilia.[#Sh. 9:13; Ebr. 5:7.]
25Wewe nidwe, nitakayekukuza, makundi mengi yakusanyikapo; nayo niliyomwagia nitayalipa mbele yao wamwogopao.[#Sh. 116:14.]
26Wanyonge sharti wale, hata washibe; sharti wamshangilie Bwana, wao wamtafutao, mioyo yenu sharti iwepo kale na kale.[#Sh. 69:33.]
27Hivyo watavikumbuka na kumrudia Bwana mapeoni pote pa nchi; yatakutambikia na kukuangukia makabila yote ya wamizimu.
28Kwani ufalme ni wake, yeye Bwana, anayewatawala wamizimu ndiye yeye.
29Wote walio wanene wa nchi watakula na kumwangukia, wote washukao uvumbini huinamia nchi mbele yake yeye, wasioweza kujipauzima ndio wao.[#Fil. 2:10.]
30Vizazi vyao navyo vitamtumikia Bwana, mambo ya Bwana yatasimuliwa kwao vijukuu.[#Yes. 53:10.]
31Watakuja, wautangaze wongofu wake kwao watakaozaliwa, kwamba: Ndiye aliyevifanya![#Sh. 110:3; Yoh. 19:30.]