The chat will start when you send the first message.
1Mheshimuni Bwana, mlio wana wa Mungu! Mheshimuni Bwana kuwa mtukufu na mnguvu![#Sh. 89:7; 103:20.]
2Liheshimuni nalo Jina lake Bwana lenye utukufu! Mtambikieni Bwana na kuvaa mapambo yapasayo Patakatifu![#Sh. 110:3.]
3Sauti ya Bwana husikilika hata baharini, Mungu mwenye utukufu ndiye apigishaye nayo ngurumo. Nako kwenye vilindi vya bahari ndiko, aliko Bwana.[#Iy. 37:2.]
4Sauti ya Bwana ni yenye nguvu, sauti ya Bwana ni yenye ukuu.
5Sauti ya Bwana huvunja miangati, kweli Bwana huivunja miangati ya Libanoni
6akiichezesha, icheze kama ndama, ile ya Libanoni na ya Sirioni icheze kama wana wa nyati.[#5 Mose 3:8-9.]
7Sauti ya Bwana hutema miali ya moto,
8Sauti ya Bwana hutetemesha nyika. Bwana aliitetemesha nayo nyika ya kule Kadesi.
9Sauti ya Bwana huzalisha kulungu, hutikisa miti ya mwituni, matawi yavunjike; kwa hiyo wote waliomo Jumbani mwake humtukuza.
10Hapo penye mafuriko ya maji Bwana alikaa juu yao; ndivyo, atakavyokaa kuwa mfalme wa kale na kale.
11Bwana atawapa nguvu walio ukoo wake, Bwana atawabariki walio ukoo wake, wapate kutengemana.[#Sh. 28:8-9.]