Mashangilio 43

Mashangilio 43

Kumtamani Mungu na Patakatifu pake.

1Niamulie, Mungu, ukinigombea kondo yangu kwao wasionipenda! Niopoe mikononi mwao wenye uwongo namo mwao wapotovu![#Sh. 26:1.]

2Kwani wewe Mungu uliye nguvu yangu, mbona umenitupa? Mbona sina budi kwenda na kusikitika, adui anaponisonga?[#Sh. 42:10.]

3Tuma mwanga wako na kweli yako, ije kuniongoza na kunipeleka kwenye mlima wako mtakatifu, Kao lako liliko.[#Sh. 15:1.]

4Niingie mwenye meza ya kumtambikia Mungu wangu, ni yule Mungu, ninayemfurahia na kumpigia vigelegele. Nitakushukuru na kukupigia zeze, Mungu uliye Mungu wangu.[#Sh. 63:6.]

5Mbona unajihangaisha, roho yangu, ukivuma ndani yangu? Mngoje Mungu na kumtazamia, kwani siku itakuja, nitakapomshukuru kwa kuokolewa nao uso wake.[#Sh. 42:5,11.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania