Mashangilio 57

Mashangilio 57

Kuomba wokovu mikononi mwa wachukivu.

2Ninamwita Mungu alioko huko juu, ni yeye Mungu atakayenimalizia mashauri yangu.

3Atamtuma toka mbinguni atakayeniokoa, naye anifokeaye atamtia soni. Mungu hutuma upole wake nao welekevu wake.

4Hapa, roho yangu ilipotua, ni penye simba, nao wanipuliziao pumzi za moto ni wana wa watu, mikuki na mishale ni meno yao, nazo ndimi zao ndio panga zenye ukali.

5Utukuke, Mungu, juu mbinguni, nazo nchi zote ziuone utukufu wako!

6Miguu yangu waliitegea matanzi, nayo roho yangu wanaiinamiza. Walinichimbia mwina mimi, wakatumbukia humo.[#Sh. 7:16.]

(8-12: Sh. 108:2-6.)

7E Mungu, moyo wangu umetulia na kushupaa, moyo wangu umetulia kweli na kushupaa; kwa hiyo na niimbe na kupiga shangwe!

8Amka, roho yangu yenye matukuzo! Amkeni, pango na zeze, niiamshe mionzi ya jua![#Sh. 16:9.]

9Kwenye makundi ya watu wako nitakushukuru, Bwana, nako kwenye wamizimu nitakuimbia.

10Kwani upole wako ni mkubwa, unafika mpaka mbinguni, nako mawinguni unafika welekevu wako.[#Sh. 36:6.]

11Utukuke, Mungu, juu mbinguni, nazo nchi zote ziuone utukufu wako!

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania