The chat will start when you send the first message.
1Niopoe, Mungu wangu, mikononi mwao walio adui zangu, ukinikingia walioniinukia, wasinifikie![#1 Sam. 19:11.]
2Niopoe mikononi mwao wafanyao mapotovu! Niokoe mikononi mwao wauao wenzao!
3Kwani unaona, jinsi wanavyoivizia roho yangu, wenye nguvu wamekusanyika, wanikamate; lakini hakuna, Bwana, nilichowapotolea, wala nilichowakosea.
4Kweli hakuna mabaya, niliyowafanyizia, tena wanapiga mbio, wajiweke tayari. Amka, unifikie, uwaone![#Sh. 44:24.]
5Nawe Bwana Mungu, uliye Mwenye vikosi, uliye Mungu wa Isiraeli, inuka, uwapatilize wamizimu wote! Usiwahurumie hata mmoja wao waliokuacha kwa upotovu tu!
6Jioni hurudi na kulia kama mbwa; ndivyo, wanavyozungukazunguka humu mjini.[#Sh. 59:15.]
7Ukiwaangalia, vinywani mwao hububujika mabaya, namo midomoni mwao zimo panga; huwaza kwamba: Yuko nani atakayetusikia?
8Lakini wewe Bwana, unawacheka, wamizimu wote unawabeza.[#Sh. 2:4.]
9Wakikaza nguvu, nitakutazamia wewe; kwani wewe, Mungu, u ngome yangu.
10Mungu wangu aliye mwenye upole hunijia mbele, yeye Mungu hunipa kuwashangilia wao walionisonga.[#Sh. 54:9.]
11Kusudi walio ukoo wangu wasivisahau, usiwaue kabisa! Wapoteze tu kwa nguvu yako, waje kutangatanga! Kisha uwakumbe, waje kuzimuni! Wewe Bwana, u ngao yangu.
12Vinywa vyao hukosa, midomo yao inaposema, sharti wanaswe na majivuno yao wakizidi kuapiza na kuogopa!
13Waishilize kwa kuwachafukia! Waishilize, watoweke! Hivyo ndivyo, yatakavyojulikana nako mapeoni kwa nchi, ya kuwa Mungu ndiye awatawalaye wa Yakobo.
14Jioni hurudi na kulia, kama ni mbwa; ndivyo, wanavyozungukazunguka humu mjini.[#Sh. 59:7.]
15Wao sharti waje kutangatanga na kutafuta chakula, kisha sharti walale pasipo kushiba!
16Ndipo, mimi nitakapoziimbia nguvu zako, asubuhi nitaushangilia upole wako, kwani umekuwa ngome yangu na kimbilio langu hapo, niliposongeka.
17Wewe uliye nguvu zangu, nitakuimbia, kwani wewe, Mungu, u ngome yangu, u Mungu wangu mwenye upole.