The chat will start when you send the first message.
1Mungu, ukitukuzwa mle Sioni, huwamo kimya, wewe ndiwe unayelipwa, watu waliyokuapia.
2Unawasikia wao wanaokuomba, kwa hiyo wenye miili ya kimtu hukujia wote.
3Manza, tulizozikora, zinatulemea, lakini wewe unayafunika nayo mapotovu yetu.
4Mwenye shangwe ni mtu, uliyemchagua, ukamkaribisha kukaa uani kwako. Ndipo, tunaposhibishwa mema ya Nyumba yako, ni kwamba: ya Kao lako lililo takatifu.[#Sh. 63:6; 84:5; 5 Mose 4:7.]
5Kwa wongofu wako unaotisha unatuitikia, wewe Mungu uliyetuokoa. U egemeo lao wote wakaao nchini hata mapeoni kwake, nalo lao wakaao mbali huko baharini.
6Uliishikiza milima kwa uwezo wako, ukajifunga nguvu zishindazo zote.
7Unautuliza uvumi wa bahari, hata uvumi wa mawimbi, nayo machafuko yao makabila ya watu.[#Sh. 89:10.]
8Kwa hiyo wakaao mapeoni kwa nchi huviogopa vielekezo vyako, nawe unawafurahisha wakaao maawioni nako machweoni kwa jua.[#Yes. 48:20.]
9Umeitokea nchi, ukainywesha, ukaichipuza sanasana, mto wake Mungu hujaa maji, ukawavunisha watu vilaji vingi, kwani hivyo ndivyo, unavyoiotesha nchi:[#Sh. 46:5.]
10matuta yake huyanywesha vizuri, mashamba yapate kulowana, mvua nyingi zikiyalegeza; ndivyo, unavyoibariki hiyo mimea yake.[#Sh. 104:13-16.]
11Magawio yako mema ya kilimo ni kama kilemba cha mwaka, nazo nyayo zako zinadondosha mafuta.
12Mbuga za nyika zimechipuka, nazo zinadondoka, vilima navyo vimejitega kushangilia.
13Nyanda zimejaa kondoo, mabonde yamefunikwa na mashamba, nao watu wanapigiana shangwe nazo nyimbo.