Mashangilio 81

Mashangilio 81

Kumshukuru Mungu na kujuta.

(Taz. Sh. 95.)

1Kwa mwimbishaji, wa kuimba kama wimbo wa wagemaji. Wa Asafu.

2Mpigieni Mungu shangwe, maana ni nguvu yetu! Mungu wa Yakobo mpigieni vigelegele!

3mwimbieni nyimbo za kumshukuru na kupiga patu! Pigeni nayo mazeze yaliayo vizuri pamoja na mapango!

4Pigeni mabaragumu, mwezi ukiandama! Hata penye mbalamwezi! Ndio sikukuu yetu.[#3 Mose 23:24,34.]

5Kwani Isiraeli alivyoagizwa, ndivyo hivyo, navyo ndivyo vimpasavyo Mungu wa Yakobo;

6ndio ushuhuda, aliouweka kwao wa Yosefu, alipotokea katika nchi ya Misri, aipige.

Hapo ndipo, niliposikia msemo, niliokuwa sijaujua:

7Huo mzigo wa begani kwake nimeuondoa, mikono yake ikaondoka kwenye makapu ya kuchukulia watu.[#2 Mose 14:10-19.]

8Uliponililia katika masongano, nimekuponya, nikakuitikia na kujificha katika mawingu yenye ngurumo, kwenye Maji ya Magomvi nikakujaribu.[#2 Mose 17:7; 4 Mose 20:13.]

9Sikilizeni, mlio wa ukoo wangu, niwaonye! Isiraeli, sharti unisikie!

10Kwako kusiwe tena na mungu mgeni! Wala usitambikie mungu wa nchi nyingine![#2 Mose 20:2-3.]

11Mungu wako, aliyekutoa katika nchi ya Misri ni mimi Bwana; kiasame kinywa chako, nikijaze![#Sh. 119:131; Mat. 5:6.]

12Lakini walio ukoo wangu hawakuisikia hiyo sauti yangu, naye Isiraeli hakutaka kunifuata mimi.

13Nikawaacha, waufuate ugumu wao wa mioyo yao, wajiendee na kuyafanya mashauri yao.[#Tume. 14:16.]

14Kama wangekuwa ukoo wangu, wangenisikia, kama wangekuwa Waisiraeli, wangezishika njia zangu,

15nami ningewainamisha upesi adui zao, mkono wangu ungewarudia wao waliowasonga.

16Wachukivu wake Bwana wangemnyenyekea, lakini wao siku zao zingekuwa za kale na kale.

17Ningewapa ngano zilizo nzuri kupita zote, wazile zizo, ningewapa hata asali za miambani, wazile, mpaka washibe.[#5 Mose 32:13.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania