The chat will start when you send the first message.
1Aliye mnyonge wa kumtegemea Bwana mpokeeni pasipo kubishana naye mawazo ya moyo![#Rom. 15:1; 1 Kor. 8:9.]
2Mwingine anayategemea ya kwamba: Vyote vinaliwa; mwingine aliye mnyonge hula maboga tu.[#1 Mose 1:29; 9:3.]
3Mwenye kula asimbeze asiyekula! Wala asiyekula asimwumbue mwenye kula! Kwani Mungu amempokea.[#Kol. 2:16.]
4Wewe u nani ukimwumbua mtumishi wa mwingine? Akiwa amesimama au akiwa ameanguka, yote humfanyizia Bwana wake mwenyewe. Lakini atainuliwa, kwani Bwana anaweza kumwinua.[#Mat. 7:1; Yak. 4:11-12.]
5Mwingine huchagulia siku za kuzitakasa, mwingine huzitakasa siku zote. Kila mtu sharti afulize kuyafuata, aliyoyatambua yeye kuwa ya kweli![#Gal. 4:10.]
6Anayezishika siku humshikia Bwana; naye asiyezishika hazishiki kwa ajili yake Bwana. Naye anayekula humlia Bwana, kwani humshukuru Mungu. Naye asiyekula hali kwa ajili yake Bwana, maana naye humshukuru Mungu.
7Kwani kwetu hakuna anayejikalia mwenyewe, wala hakuna anayejifia mwenyewe.
8Kwani tunapokaa humkalia Bwana, tena tunapokufa humfia Bwana. Basi, ikiwa twakaa au ikiwa twafa, sisi tu wa Bwana.[#Gal. 2:20; 1 Tes. 5:10.]
9Kwani kwa hiyo Kristo alikufa, akawa mzima tena, apate kuwatawala waliokufa nao wanaoishi.*
10Lakini wewe unamwumbuaje ndugu yako? Au wewe unambezaje ndugu yako? Kwani sisi sote tutatokezwa mbele ya kiti cha uamuzi cha Mungu.[#Mat. 25:31-32; Tume. 10:42; 17:31; 2 Kor. 5:10.]
11Kwani imeandikwa: Bwana anasema:
Kwa hivyo, nilivyo Mwenye uzima, wote watanipigia magoti,
nazo ndimi zote zitamwungama Mungu.
12Basi, kwa hiyo sisi sote kila mmoja atajisemea mwenyewe mbele ya Mungu.[#Gal. 6:5.]
13Basi, tusiumbuane wenyewe tena, ila mjue, ya kuwa ni kuumbua, mtu akimtegea ndugu yake, ajigonge au ajikwae!
14Nimeyajua, nikayashika kabisa moyoni kwa kuwa na Bwana Yesu, ya kuwa: hakuna kilicho chenye mwiko hivyo, kilivyo; lakini mtu akikiwazia kuwa chenye mwiko, basi, kwake yeye ni chenye mwiko.[#Mat. 15:11; Tume. 10:15; 1 Kor. 10:30; Tit. 1:15.]
15Lakini ndugu yako akisikitishwa, wewe ukila, basi, umekwisha kuuacha upendo. Tena ukila usimponze mwenzio, ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.[#1 Kor. 8:11-13.]
16Yaliyo mema kwenu yaangalieni, yasibezwe![#Tit. 2:5.]
17Kwani ufalme wake Mungu sio kula na kunywa, ila wongofu na utengemano na ushangilio unaopatikana katika Roho takatifu.[#Luk. 17:20; Ebr. 13:9.]
18Kwani anayemtumikia Kristo na kuyatenda mambo haya humfalia Mungu, tena hupendwa na watu.
19Basi, kwa hiyo tukaze kuyafuata mambo yanayopatanisha, ni yaleyale yanayotujenganisha![#Rom. 12:18; 15:2.]
20Usiitengue kazi ya Mungu kwa ajili ya chakula! Kweli, vyote hutakata; lakini mtu akivila na kujikwaa, vimekwisha kumponza.[#Rom. 14:14.]
21Ni vizuri, usile nyama, wala usinywe pombe, wala usifanye cho chote kinachomkwaza ndugu yako.[#1 Kor. 8:13.]
22Wewe unayoyategemea moyoni, yategemee hata mbele ya Mungu! Mwenye shangwe ni yule asiyejipatia hukumu kwa ajili yao yale, aliyoyaona kuwa ya kufaa.
23Lakini mtu akila mwenye mashaka amekwisha kujipatia hukumu, kwani hakula kwa kumtegemea Mungu. Nayo yote, mtu anayoyafanya pasipo kumtegemea Mungu, ndiyo makosa.[#Tit. 1:15.]