The chat will start when you send the first message.
1*Kwa hiyo huna la kujikania, wewe uwaye yote, ukiumbua wengine. Kwani kwa hilo, unalomwumbua mwingine, unajionea patilizo mwenyewe. Kwani wewe muumbuaji unayafanya yayo hayo.[#Mat. 7:2; Yoh. 8:7.]
2Nasi twajua, ya kuwa wenye mambo kama hayo Mungu hwaumbua kweli, wajulike, walivyo.
3Lakini wewe ukiumbua wengine walio wenye mambo unayoyafanya, kisha unayafanya yaleyale, unajiwaziaje, ya kwamba wewe utaipona hukumu ya Mungu?
4Au unaubeza wema na uvumilivu na ungojevu wake mwingi? Hujui, ya kuwa wema wa Mungu unakuonyesha njia ya kujuta?[#2 Petr. 3:15.]
5Lakini wewe mwenye moyo mgumu unaokataa kujuta unajilimbikia mwenyewe makali, yakupate siku ya makali, hukumu inayopasa itakapofunuliwa na Mungu.
6Ndipo, atakapomlipa kila mtu, kama matendo yake yalivyo:[#Mat. 16:27.]
7wale wasiochoka kufanya mema kwa kutafuta utukufu na heshima na mengine yasiyooza, hao watapewa uzima wa kale na kale.[#Yoh. 5:29; 2 Kor. 5:10.]
8Lakini wale wachokozi wanaokataa kuyatii yaliyo ya kweli kwa kupendezwa na upotovu, hao watapata makali yenye moto.[#2 Tes. 1:8.]
9Maumivu na masongano yataupata moyo wa kila mtu anayefanya maovu, kwanza Wayuda, kisha Wagriki nao.[#Rom. 1:16; 3:9.]
10Lakini utukufu na heshima na utengemano ndio, atakaoupata kila anayefanya mema, kwanza Wayuda, kisha Wagriki nao.
11Kwani Mungu hautazami uso wa mtu.*[#Tume. 10:34; 1 Petr. 1:17.]
12Kwani wote waliokosa wasipoyajua Maonyo huangamia tu pasipo Maonyo, nao wote waliokosa wakiyajua Maonyo hao watahukumiwa kwa Maonyo.
13Kwani walio wenye wongofu machoni pa Mungu sio wenye kuyasikia Maonyo, ila wenye kuyafanya Maonyo ndio watakaopewa wongofu.[#Mat. 7:21; 1 Yoh. 3:7.]
14Kwani wamizimu wasiopata maonyo wakiyafanya mambo ya Maonyo wenyewe, basi, hao wasiopata maonyo mioyo yao ndiyo iliyokuwa maonyo yao.[#Tume. 10:35.]
15Hao wanaonyesha, ya kuwa kazi, Maonyo yanayoitaka, imeandikwa mioyoni mwao; nayo, wanayoyajua mioyoni, huwashuhudia, ndiyo mawazo ya mioyo yanayoinukiana, nayo mengine yanayokaniana.[#Rom. 1:32.]
16Haya yatajulikana siku ile, Mungu atakapompa Kristo Yesu kuyaumbua yaliyofichwa na watu. Huu ndio Utume mwema, niliopewa.[#Mbiu. 12:14.]
17Angalia, wewe unayeitwa Myuda, unayatumia Maonyo ya kupumzikia ukijivunia kwamba: Mungu ninaye!
18Kweli unayatambua, anayoyataka, kisha ukayatenga yaliyo mepesi nayo yaliyo magumu, kwa kuwa umefundishwa mambo ya Maonyo.
19Hivyo unajiwazia mwenyewe kuwa kiongozi wa vipofu na mwanga wao wakaao gizani,[#Mat. 15:14.]
20ukataka kuonya wajinga na kufundisha wachanga, kwani Maonyo yalikuwa yamekuonyesha, jinsi mtu anavyopata utambuzi na ukweli.[#2 Tim. 3:5.]
21Je? Wewe unayefundisha mwingine, hujifundishi mwenyewe? Je? Wewe unayetangaza, wasiibe, huibi mwenyewe?[#Sh. 50:16-21; Mat. 23:3-4.]
22Je? Wewe unayesema, wasizini, huzini mwenyewe? Je? Wewe unayechukizwa na vinyago vya kutambikia, huvinyang'anyi nyumbani mwao mwa kuombea?
23Je? Wewe, unayejivunia kwamba: Ninayo Maonyo, humbezi Mungu kwa kuyakosea Maonyo yake?
24Kwani Jina lake Mungu hutukanwa kwa wamizimu kwa ajili yenu ninyi, kama ilivyoandikwa.[#Yes. 52:5; Ez. 36:20.]
25Kwani kutahiri kunafaa, kama unayashika Maonyo. Lakini ukiyakosea Maonyo, kutahiriwa kwako ni kwa bure, utakuwa tena kama mtu asiyetahiriwa.[#Yer. 4:4; 9:24-25.]
26Basi, asiyetahiriwa akiyafuata maongozi ya Maonyo hatawaziwa kuwa kama mwenye kutahiriwa, ijapo hakutahiriwa?[#Gal. 5:6.]
27Kwa hiyo mtu asiyetahiriwa aliye vivyo hivyo, alivyozaliwa, akiyatimiza Maonyo atakuumbua wewe uliye mwenye Maandiko na mwenye tohara, ukiwa unayakosea Maonyo
28Kwani Myuda si yeye anayejulikana kwa nje, ya kuwa ni Myuda, nako kutahiriwa siko kule kunakojulikana nje mwilini.[#Yoh. 8:39.]
29Lakini aliye Myuda huko ndani kusikoonwa na watu, yeye ni Myuda. Nako kutahiriwa, kama ilivyoandikwa, siko; kwenye kweli ndiko kutahiriwa kwa moyo kunakowezekana kwa nguvu ya Roho; nako kutasifiwa, lakini siko kwa watu, ila kwa Mungu[#5 Mose 30:6; Kol. 2:11.]