Wimbo mkuu 5

Wimbo mkuu 5

1“Ninaingia bustanini pangu, umbu langu na mchumba wangu,

niunge manemane na manukato yangu,

nile masega yangu pamoja na asali yangu,

ninywe mvinyo yangu na maziwa yangu.

Nanyi wenzangu, leni, nyweni, mpaka mleweshwe na upendo!

Mpenzi mke anamtunukia mpendwa wake mume.

2Nililala usingizi, lakini moyo ulikuwa macho;

mara nikasikia, mpendwa wangu akigonga mlango:

“Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu,

hua yangu, mwenzangu atakataye!

Kwa kuwa nimejazwa umande kichwani pangu,

kwa kuwa misuko ya nywele zangu imejaa unyevu wa usiku.”

3Nikajibu: Nimekwisha kuivua kanzu yangu, nitaivaaje tena?

Nikaisha kuiogesha miguu yangu, nitawezaje kuichafua tena?

4Ndipo, mpendwa wangu alipoutia mkono wake tunduni,

moyo wangu ukarukaruka ndani kwa ajili yake.

5Nikainuka kumfungulia yeye mpendwa wangu,

manemane yalipokuwa yanachuruzika mikononi pangu,

navyo vidole vyangu vikadondokea manemane

6Lakini nilipokwisha kumfungulia mpendwa wangu,

alikuwa ametoweka kabisa, yeye mpendwa wangu.

Hapo aliposema, roho yangu ilitaka kuzimia,

kwa hiyo nikamtafuta, lakini sikumwona, nikamwita, lakini hakunijibu.

7Walinzi wazungukao mjini waliponiona wakanipiga na kuniumiza,

wakanivua mtandio wangu wale walinzi wa boma.

Mkimwona mpendwa wangu mtampasha habari gani?

Ya kuwa mimi nimeugua kwa upendo tu!

Mpendwa wangu ni mweupe sana, tena mwekundu,

11Mkikitazama kichwa chake, ni kama dhahabu tupu,

misuko ya nywele zake nayo ni makuti yaning'iniayo,

12Macho yake kama ya hua waliopo penye vijito vya maji,

hujiogesha katika maziwa, huwapo na kuchangamka sana.

13Mashavu yake ni kama matuta yaliyopandwa manukato,

namo juu mna vijanijani vinukavyo vizuri;

midomo yake ni nyinyoro zidondokazo manemane ya majimaji.

14Mikono yake ni vigogo vya dhahabu zilizotiwa vito vingi vya Tarsisi,

tumbo lake ni urembo wa meno ya tembo uliofunikwa na vito vya safiro.

15Paja zake ni nguzo za mawe meupe juu ya misingi ya dhahabu tupu;

ukimtazama, anafanana na Libanoni, ni mtukufu kama miangati.

16Kinywa chake husema matamu tu, yaliyo yake yote pia hupendeza.

Ndivyo mpendwa wangu alivyo, ndivyo, mwenzangu alivyo,

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania