Tito 1

Tito 1

Anwani.

1Mimi Paulo ni mtumwa wa Mungu na mtume wa Yesu Kristo kwamba: Waliochaguliwa na Mungu wapate kumtegemea na kuyatambua yaliyo ya kweli; ndiyo yaliyotufundisha kumcha Mungu na kuungojea uzima wa kale na kale.

2Huu ndio wa kiagio, Mungu asiyesema uwongo alichokiweka siku za kale mwenyewe,

3lakini siku zake zilipotimia, akalifufua Neno lake akiitangaza mbiu, niliyopewa nami kuipiga, kama nilivyoagizwa na mwokozi wetu Mungu.[#Ef. 1:9-10; 1 Tim. 1:1,11.]

4Nakuandikia wewe, Tito, maana u mwanangu wa kweli kwa hivyo, tulivyo mmoja kwa kumtegemea Mungu. Upole ukukalie na utengemano unaotoka kwa Mungu Baba na kwa mwokozi wetu Kristo Yesu![#1 Tim. 1:2.]

Iwapasayo wazee na wakaguzi.

5Kwa sababu hii nilikuacha katika Kreta, uyatengeneze yaliyosalia, uiweekee miji yote wazee, kama nilivyokuagiza:[#Tume. 14:23.]

6akiwa mtu asiye na neno la kumkamia, aliye mume wa mke mmoja, tena mwenye watoto waelekevu wasiosingiziwa kuwa waasherati wala wabezi.[#1 Tim. 3:1-7,10.]

7Kwani mkaguzi imempasa kuwa mtu asiye na neno la kumkamia, maana humtunzia Mungu walio wake. Asiwe mwenye kujipendeza wala mwenye makali wala mywaji wala mgomvi wala mwenye machumo mabaya![#1 Kor. 4:1; 2 Tim. 2:24.]

8Ila sharti awe mpenda wageni na mpenda mema na mwerevu wa kweli na mwongofu na mcha Mungu na mwenye kujikataza mabaya!

9Sharti ashikamane na kulitegemea Neno, tulilofundishwa, maana ajue kuituliza mioyo yao wale, atakaowafundisha njia ya uzima, tena ajue kuwashinda hata wabishi.

Wapotevu walivyo.

10Kwani kuna wengi wasiotii, walio wapuzi na wapotevu. Wapitao wengine ndio wale waliotahiriwa;

11hupaswa na kufumbwa vinywa, kwani hufudikiza nyumba nzima wakifundisha yasiyopasa, wapate mali; hili ndilo chumo lao baya.[#2 Tim. 3:6.]

12Mfumbuaji wa kwao aliyekuwa mwenzao wenyewe alisema: Wakreta ndio waongo kabisa, ni nyama waovu, ni matumbo mavivu;

13ushuhuda huu ni wa kweli. Kwa sababu hii uwagombeze kwa ukali, wapate kupona na kumtegemea Mungu,[#2 Tim. 4:2.]

14wasiyashike masimulio ya Kiyuda, wala maagizo ya watu waliogeuka na kuyaacha yalio ya kweli.[#1 Tim. 4:7.]

15Wenye kutakata mioyo, vyote huwatakatia; lakini wenye mioyo michafu wasiomtegemea Mungu hakuna kiwatakiacho, maana hata mawazo yao ni machafu, mioyo isijue tena yatakatayo.[#Mat. 15:11; Rom. 14:20.]

16Huungama kwamba: Tumemjua Mungu, lakini kwa matendo yao hakuna kuwa wake. Kwani hutapisha, kwa kuwa hawatii, hawafai kabisa kufanya kazi yo yote iliyo njema.[#2 Tim. 3:5.]

Swahili Roehl Bible 1937 © Bible Society of Tanzania, 1937.
Published by: Bible Society of Tanzania