The chat will start when you send the first message.
1Wakumbushe wajinyenyekeze penye wakuu na wenye nguvu, wamtii na kujiweka tayari kufanya kazi njema zo zote![#Rom. 13:1; 1 Petr. 2:13.]
2Wasitukane mtu, wala wasichokoze wenyewe, ila wajionyeshe kuwa wenye mambo yapasayo, wawaendee watu wote kwa upole kabisa![#Fil. 4:5.]
3Kwani hata sisi kale tulikuwa wapumbavu waliokataa kutii; tulikuwa tumepotea, tukazitumikia tamaa nyingi zilizotupendeza, tukaendelea kuwa wenye maovu na wivu na machukivu ya kuchukiana sisi kwa sisi.[#1 Kor. 6:11; Ef. 2:2; 5:8.]
4*Ndipo, ulipotutokea utu wake mwokozi na Mungu wetu aliyetupenda sisi watu,[#Tit. 2:11.]
5akatuokoa sisi, lakini si kwa sababu ya matendo ya wongofu, tuliyofanya sisi; ila kwa huruma yake yeye alituponya akituosha maji ya kutuzaa mara ya pili, tukawa watu wapya kwa kupewa Roho takatifu;[#Yoh. 3:5; Ef. 2:8-9; 5:26.]
6hii ndiyo aliyotumiminia, ikatifurikia, alipomtuma mwokozi wetu Yesu Kristo.[#Yoe. 2:28.]
7Kwa mema yake yeye, aliyotugawia, tukapata wongofu, tukawekewa nasi urithi wetu penye uzima wa kale na kale, kama tunavyongojea.*
8Hili neno ni la kweli. Nami nataka, mambo haya uyafundishe kwa nguvu ya kuwashinda, maana wale waliomtegemea Mungu wazitunze kazi zao, ziwe nzuri kuliko za wengine. Haya ni mazuri, nayo huwafalia watu.[#Tit. 3:14.]
9Lakini mabishano ya upuzi na mambo ya wakale na machokozi na magomvi ya miiko uyaache! Kwani hayafai kitu, ni ya bure tu.[#1 Tim. 4:7.]
10Mtu mzushi mwonye mara moja, hata mara mbili! Asipoonyeka, mwepuke![#Mat. 18:15-17; 2 Yoh. 10.]
11Ujue: Mtu aliye hivyo amekwisha kutengeka, tena hujipatia hukumu mwenyewe kwa kukosa kwake.[#1 Tim. 6:4-5.]
12Nitakapomtuma kwako Artema au Tikiko, jikaze kuja kwangu huku Nikopoli! Kwani ndiko, ninakotaka kuzimaliza siku hizi za kipupwe.[#2 Tim. 4:12.]
13Akina Zena aliye mjuzi wa Maonyo na Apolo watume upesi, waende zao; lakini uwatunzie vema, wasikose yawapasayo njiani![#Tume. 18:24; 1 Kor. 3:5-6.]
14Hapo wa kwetu nao wajifunze kufanya kazi zilizo nzuri kuliko za wengine! Ikiwa wanatakwa, na wapatie wengine yatakayowatunza, wasifanane na miti isiyozaa![#Tit. 2:14; Mat. 7:19; Ef. 4:28.]
15Wanakusalimu wote walio pamoja nami. Wasalimu wanaotupenda kwa kuwa wenye kumtegemea Mungu! Upole uwakalie ninyi nyote! Amin.