The chat will start when you send the first message.
1Kisha yule malaika aliyesema na mimi akarudi, akaniamsha kama mtu anayeamshwa katika usingizi wake.
2Akaniuliza: Unaona nini? Nikasema: Nimechungulia, nikaona kinara kilicho cha dhahabu tupu, nacho chombo chake cha mafuta kilikuwa juu yake, nazo taa zake zilikuwa saba, tena penye hizo taa zilizoko juu yake palikuwa na mirija saba ya kutilia mafuta.[#Yer. 1:11,13; Amo. 8:2; 2 Mose 25:31-40.]
3Kando yake iko michekele miwili, mmoja kuumeni penye chombo cha mafuta, mmoja kushotoni pake.
4Nikasema na kumwuliza malaika aliyesema na mimi kwamba: Vya nini hivi, Bwana wangu?
5Malaika aliyesema na mimi akajibu akiniambia: Je? Hujui, kama hivi ni vya nini? Nikasema: Sijui, Bwana wangu.
6Akajibu akiniambia kwamba: Hili ndilo neno la Bwana lililomjia Zerubabeli la kwamba: Haitafanyika kwa vikosi wala kwa nguvu, ila kwa Roho yangu; ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
7Nawe wewe mlima mkubwa ndiwe nani? Mbele ya Zerubabeli utageuka kuwa nchi tambarare, upate kulitoa jiwe la juu pembeni, wakimshangilia kwamba: Ppngezi! Pongezi![#Sh. 122:6.]
8Ndipo, neno la Bwana liliponijia la kwamba:
9Mikono yake Zerubabeli imeweka msingi wa Nyumba hii, nayo mikono yake ndiyo itakayoimaliza. Ndipo, utakapojua, ya kuwa Bwana Mwenye vikosi amenituma kwenu.[#Ezr. 3:8; 6:14-16; Zak. 2:9-11.]
10Kwani walioibeua siku ya mambo madogo ndio watakaofurahi wakiiona timazi mkononi mwa Zerubabeli; hizi taa saba ndio macho ya Bwana, ndiyo yanayotembea katika nchi hii nzima.[#Hag. 2:3; Zak. 3:9.]
11Nikajibu na kumwuliza: Hii michekele miwili iliyoko kuumeni kwa kinara na kushotoni kwake ni ya nini?
12Nikaanza kusema mara ya pili na kumwuliza: Vichala hivi viwili vya michekele vilivyoko kando ya mirija ya dhahabu inayoyapeleka hayo mafuta yao ya dhahabu toka juu maana yao nini?
13Akaniambia kwamba: Je? Huijui maana yao? Nikasema: Siijui, Bwana wangu.
14Akaniambia: Hivi ndio wana wawili waliopakwa mafuta wanaosimama kwake Bwana wa nchi hii yote nzima.[#Ufu. 11:4.]