1 Mambo ya Nyakati 4

1 Mambo ya Nyakati 4

Wazawa wa Yuda

1Wana wa Yuda; Peresi, na Hesroni, na Karmi, na Huri, na Shobali.[#Mwa 38:29; 46:12; Hes 26:20,21; Rut 4:18]

2Na Reaya, mwana wa Shobali, akamzaa Yahathi; na Yahathi akawazaa Ahumai, na Lahadi. Hizo ndizo jamaa za Wasorathi.

3Na hawa ndio wana wa babaye Etamu; Yezreeli, na Ishma, na Idbashi; na dada yao aliitwa jina lake Haselelponi;

4na Penueli, babaye Gedori, na Ezeri, babaye Husha. Hao ndio wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata, babaye Bethlehemu.

5Naye Ashuri, babaye Tekoa, alikuwa na wake wawili, Hela na Naara.

6Naye Naara akamzalia Ahuzamu, na Heferi, na Temeni, na Ahashtari. Hao ndio wana wa Naara.

7Na wana wa Hela walikuwa Serethi, na Ishari, na Ethnani.

8Na Hakosi akawazaa Anubu, na Sobeba, na jamaa za Aharheli, mwana wa Harumu.

9Naye Yabesi alikuwa mwenye heshima kuliko nduguze; na mamaye akamwita Yabesi, akisema, Ni kwa sababu nilimzaa kwa huzuni.[#Mwa 34:19; Zab 112:6; Mit 10:7; Mwa 3:16]

10Huyo Yabesi akamlingana Mungu wa Israeli, akisema, Lau kwamba ungenibariki kweli kweli, na kuipanua mipaka yangu, na mkono wako ukawa pamoja nami, nawe ungenilinda nisipatwe na maovu wala madhara! Naye Mungu akamjalia hayo aliyoyaomba.[#Mwa 12:8; 1 Nya 16:8; Ayu 12:4; 22:27; Isa 12:4; 1 Fal 3:7-13; Zab 21:4; 65:2; Mt 7:7-11]

11Naye Kelubu, nduguye Shuha, akamzaa Mehiri, aliyekuwa babaye Eshtoni.

12Na Eshtoni akamzaa Beth-Rafa, na Pasea, na Tehina, babaye Ir-nahashi. Hao ni watu wa Reka.

13Na wana wa Kenazi; Othnieli, na Seraya; na wana wa Othnieli; Hathathi na Meonothai.[#Yos 15:17; #4:13 Makala ya Kiebrania haina Meonothai.]

14Na Meonothai akamzaa Ofra; na Seraya akamzaa Yoabu, babaye Ge-harashimu; kwani hao walikuwa mafundi stadi.[#Neh 11:35; #4:14 Maana yake ‘Bonde la Wahunzi’.]

15Na wana wa Kalebu, mwana wa Yefune; Iru, na Ela, na Naamu; na wana wa Ela; na Kenazi.

16Na wana wa Yehaleleli; Zifu, na Zifa, na Tiria, na Asareli.

17Na wana wa Ezrahi; Yetheri, na Meredi, na Eferi, na Yaloni; na Miriamu akamzalia na Shamai, na Ishba, babaye Eshtemoa.

18Na mkewe Myahudi akawazaa Yeredi, babaye Gedori, na Heberi, babaye Soko, na Yekuthieli, babaye Zanoa. Na hawa ndio wana wa Bithia, binti Farao, ambaye Meredi alimwoa.

19Na wana wa mkewe Hodia, dada yake Nahamu, walikuwa babaye Keila, Mgarmi, na Eshtemoa, Mmaaka.

20Na wana wa Shimoni; Amnoni, na Rina, na Ben-hanani, na Tiloni. Na wana wa Ishi; Zohethi, na Ben-zohethi.

21Wana wa Shela, mwana wa Yuda; Eri, babaye Leka, na Laada, babaye Maresha, na jamaa zao wa ukoo wa wafuma nguo za kitani safi, wa ukoo wa Ashbea;[#Mwa 38:1]

22na Yokimu, na watu wa Kozeba, na Yoashi, na Sarafi waliokuwa na mamlaka katika Moabu, na Yashubi-lehemu. (Na taarifa hizi ni za zamani sana).[#2 Sam 8:2]

23Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake.

Wazawa wa Simeoni

24Wana wa Simeoni; Yemueli, na Yamini, na Yakini, na Sohari, na Shauli;

25na mwanawe huyo ni Shalumu, na mwanawe huyo ni Mibsamu, na mwanawe huyo ni Mishma.

26Na wana wa Mishma; mwanawe huyo ni Hamueli, na mwanawe huyo ni Zakuri, na mwanawe huyo ni Shimei.

27Naye Shimei alikuwa na wana wa kiume kumi na sita, na wana wa kike sita; lakini nduguze walikuwa hawana watoto wengi, tena jamaa yao yote haikuongezeka sana kama wana wa Yuda.

28Nao wakakaa huko Beer-sheba, na Molada, na Hasar-shuali;

29na huko Bilha, na Esemu, na Toladi;

30na huko Bethueli, na Horma, na Siklagi;

31na huko, Beth-markabothi, na Hasar-susimu, na Bethbiri, na Shaaraimu. Hiyo ndiyo miji yao hadi wakati wa kutawala kwa Daudi.

32Na vijiji vyao vilikuwa Etamu, na Aini, na Rimoni, na Tokeni, na Ashani, miji mitano,

33na vijiji vyote vilivyoizunguka miji iyo hiyo, mpaka Baali. Hayo ndiyo makao yao, na hati ya nasaba yao wanayo.

34Naye Meshobabu, na Yamleki, na Yosha, mwana wa Amazia;

35na Yoeli, na Yehu, mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli;

36na Elioenai, na Yaakoba, na Yeshohava, na Asaya, na Adieli, na Yesimieli, na Benaya;

37na Ziza, mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya mwana wa Shimri, mwana wa Shemaya;

38hao waliotajwa majina yao ndio waliokuwa wakuu katika jamaa zao; na koo za baba zao zikaongezeka sana.

39Basi wakaenda mpaka maingilio ya Gedori, naam, mpaka upande wa mashariki wa bonde hilo, ili kuwatafutia kondoo wao malisho.

40Wakaona malisho ya unono, mazuri, na nchi yenyewe ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani; kwani waliokaa huko zamani walikuwa watu wa Hamu.[#Mwa 9:22; 10:6; Zab 78:51]

41Na hao walioandikwa majina yao waliingia huko katika siku za Hezekia, mfalme wa Yuda, na kuziharibu hema zao, pamoja na hao Wameuni waliokuwa wakiishi huko, wakawaangamiza kabisa, hata siku hii ya leo, nao wakakaa huko badala yao; kwa sababu huko kulikuwa na malisho kwa kondoo wao.[#2 Fal 18:8]

42Na baadhi yao, wana wa Simeoni wapatao watu mia tano, wakaenda mpaka mlima Seiri, na majemadari wao walikuwa Pelatia, na Nearia, na Refaya, na Uzieli, wana wa Ishi.

43Nao wakawaua Waamaleki waliokuwa wamenusurika, wakakaa huko, hata siku hii ya leo.[#1 Sam 15:8; 30:17; 2 Sam 8:12]

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya