The chat will start when you send the first message.
1Basi Wafilisti wakapigana na Israeli; nao watu wa Israeli wakawakimbia Wafilisti, wakauawa katika mlima wa Gilboa.[#1 Sam 28:1,15; 29:1; 1 Nya 10:1; 1 Sam 28:4]
2Wafilisti wakamfuatia sana Sauli na wanawe, Wafilisti wakawaua Yonathani, na Abinadabu, na Malkishua, wana wa Sauli.[#1 Nya 8:33]
3Tena vita vilikuwa vikali sana juu ya Sauli, na wapiga upinde wakampata; hata akafadhaika sana kwa sababu ya wapiga upinde.[#2 Sam 1:6]
4Ndipo Sauli akamwambia yule mchukua silaha zake, Futa upanga wako, unichome nao; wasije watu hawa wasiotahiriwa wakanichoma, na kunisimanga. Lakini huyo mchukua silaha zake akakataa; kwa sababu aliogopa sana. Basi Sauli akautwaa upanga wake, akauangukia.[#Amu 9:54; 1 Sam 14:6; 17:26; 2 Sam 1:10]
5Na mchukua silaha zake alipoona ya kuwa Sauli amekufa, yeye naye akauangukia upanga wake, akafa pamoja naye.
6Hivyo Sauli akafa, na wanawe watatu, na mchukua silaha zake, na watu wake wote pamoja siku iyo hiyo.[#1 Sam 12:25; 1 Nya 10:6; Rum 6:23]
7Kisha watu wa Israeli waliokuwa upande wa pili wa bonde lile, na ng'ambo ya Yordani, walipoona ya kuwa watu wa Israeli wamekimbia, na ya kuwa Sauli na wanawe wamekufa, wakaiacha miji yao, wakakimbia; nao Wafilisti wakaenda wakakaa humo.
8Hata ikawa, siku ya pili yake, Wafilisti walipokwenda kuwateka nyara waliouawa, walimwona Sauli na wanawe watatu wameanguka juu ya mlima wa Gilboa.
9Wakamkata kichwa, wakamvua silaha zake, wakapeleka wajumbe kwenda nchi ya Wafilisti pande zote, ili kutangaza habari nyumbani mwa sanamu zao, na kwa watu.[#2 Sam 1:20]
10Wakaziweka silaha zake nyumbani mwa Maashtorethi; wakakitundika kiwiliwili chake katika ukuta wa Beth-sheani.[#1 Sam 21:9; Amu 2:13; Yos 17:11; Amu 1:27]
11Na wenyeji wa Yabesh-gileadi waliposikia habari zake, jinsi hao Wafilisti walivyomtenda Sauli,
12wakainuka mashujaa wote, wakaenda usiku kucha, wakautwaa mwili wake Sauli, na miili ya wanawe, na kuiondoa ukutani kwa Beth-sheani nao wakaja Yabeshi, na kuiteketeza huko.[#1 Sam 11:1-11; 2 Sam 2:4-7; 2 Nya 16:14; Yer 34:5; Amo 6:10]
13Kisha wakaitwaa mifupa yao, na kuizika chini ya mkwaju huko Yabeshi, nao wakafunga siku saba.[#2 Sam 21:12-14; Mwa 50:10; Ayu 2:13]