2 Mambo ya Nyakati 4

2 Mambo ya Nyakati 4

Mapambo ya hekalu

1Tena akafanya madhabahu ya shaba, dhiraa ishirini urefu wake, na dhiraa ishirini upana wake, na dhiraa kumi kwenda juu kwake.[#Kut 27:1; 1 Fal 9:25; 2 Fal 16:14; Eze 43:13]

2Tena akaifanya bahari ya kusubu, dhiraa kumi toka ukingo hadi ukingo, ya mviringo, na kwenda juu kwake ilikuwa dhiraa tano; na uzi wa dhiraa thelathini kuizunguka kabisa.[#Kut 30:18; 1 Fal 7:23; #4:2 ‘Tangi la maji’]

3Na chini yake palikuwa na mifano ya fahali, walioizunguka pande zote, kwa dhiraa kumi, wakiizunguka pande zote ile bahari. Fahali walikuwa safu mbili, wakayeyushwa hapo ilipoyeyushwa hiyo bahari.[#1 Fal 7:24; #4:3 Au, maboga (1 Fal 7:24).; #4:3 Tazama 4:2.; #4:3 Tazama 4:2.]

4Ikakaa juu ya ng'ombe kumi na wawili, watatu wakitazama kaskazini, na watatu wakitazama magharibi, na watatu wakitazama kusini, na watatu wakitazama mashariki; na bahari iliwekwa juu yao, na pande zao za nyuma zote zilikuwa ndani.

5Na unene wake ulikuwa nyanda nne, na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi elfu tatu, kukaa ndani yake.[#1 Fal 7:26; #4:5 Tazama 2:10.]

6Akafanya na birika kumi, akaziweka tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto, za kuoshea; ndizo walizooshea mambo ya kafara; lakini hiyo bahari ilikuwa ya makuhani ya kuogea.[#1 Fal 7:38; Ebr 9:9]

7Alivitengeneza vinara vya taa kumi vya dhahabu, kama vilivyoagiziwa; akavitia hekaluni, vitano upande wa kulia, na vitano upande wa kushoto.[#1 Fal 7:49; Kut 25:31]

8Akatengeneza na meza kumi, akazitia hekaluni, tano upande wa kulia, na tano upande wa kushoto. Kisha akafanya mabakuli mia moja ya dhahabu.[#1 Fal 7:48]

9Tena akatengeneza ua wa makuhani, na ua mkubwa, nayo milango yake, akaifunikiza kwa shaba milango yake.[#1 Fal 6:36]

10Nayo bahari akaiweka upande wa kulia kwa mashariki, kuelekea kusini.[#1 Fal 7:39]

11Na Huramu akatengeneza vyungu, sepetu, na mabeseni.[#1 Fal 7:40]

Basi Huramu akamaliza kufanya hiyo kazi, aliyomfanyia mfalme Sulemani ya nyumba ya Mungu;

12zile nguzo mbili, na mabakuli, na mataji mawili yaliyokuwa juu ya nguzo; nazo nyavu mbili za kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yaliyokuwa juu ya nguzo;[#1 Fal 7:41]

13na makomamanga mia nne ya nyavu mbili; safu mbili za makomamanga kwa kila wavu, kuyafunika mabakuli mawili ya mataji yalikuwa juu ya nguzo.[#Kut 28:33,34; 1 Fal 7:20; Wim 4:13; Yer 52:23]

14Akatengeneza vitako, akatengeneza na mabeseni juu ya vitako;[#1 Fal 7:27,43]

15mafahali kumi na wawili chini yake.

16Vyungu, pia sepetu, nyuma na vyombo vingine vyote, Huram-abi akamtengenezea mfalme Sulemani kwa ajili ya nyumba ya BWANA, vilikuwa vya shaba iliyong'arishwa.[#1 Fal 7:14,45; #4:16 Au, Huramu babaye.]

17Katika uwanda wa Yordani ndipo mfalme alipovisubu, katika udongo mzito kati ya Sukothi na Sereda.[#1 Fal 7:46]

18Ndivyo Sulemani alitengeneza vyombo hivi vikiwa vingi sana, uzani wa shaba lliyotumika haukujulikana.[#1 Fal 7:47]

19Basi Sulemani akavifanya vyombo vyote vilivyokuwamo nyumbani mwa Mungu, madhabahu ya dhahabu pia, nazo meza, ambazo juu yake iliwekwa mikate ya wonyesho;[#1 Fal 7:48-50; 2 Fal 24:13; Yer 28:3; Dan 5:2,3; Kut 25:30; 1 Nya 28:16]

20na vinara na taa zake, ziwake kama ilivyoagizwa mbele ya chumba cha ndani, vya dhahabu iliyosafika;[#Kut 27:20,21]

21na maua, na taa, na makoleo, ya dhahabu, ndiyo dhahabu bora;[#Kut 25:31; 37:20; 1 Fal 6:18-35]

22na mikasi, na mabakuli, na miiko, na vyetezo, vya dhahabu iliyosafika; na kwa habari za mahali pa kuingia nyumbani, milango yake ya ndani ya patakatifu pa patakatifu, na milango ya nyumba, yaani ya hekalu, ilikuwa ya dhahabu.[#1 Fal 6:31]

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya