The chat will start when you send the first message.
1Musa akawaita Israeli wote, akawaambia, Enyi Israeli, zisikieni amri na hukumu nisemazo masikioni mwenu leo, mpate kujifunza na kuzizingatia.
2BWANA, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu.[#Kut 19:5; 24:7,8; Kum 4:23; Ebr 8:6-13; 9:19-23]
3BWANA hakufanya agano hili na baba zetu, bali na sisi, yaani, sisi sote tuliopo hapa, tu hai.[#Mt 13:17; Ebr 8:9]
4BWANA alisema nanyi uso kwa uso mlimani, kutoka kati ya moto;[#Kut 19:9,19; 20:22; Kum 4:33,36; 34:10]
5(nami wakati ule nikiwa nimesimama kati ya BWANA na ninyi, ili kuwaonesha neno la BWANA; maana, mliogopa kwa sababu ya ule moto, wala hamkupanda mlimani); naye akasema,[#Kut 19:16; 20:21; Hes 16:48; Zab 106:23; Yer 30:21; Gal 3:19; Ebr 12:18,19; Kut 24:2]
6Mimi ni BWANA, Mungu wako, niliyekutoa katika nchi ya Misri, katika nyumba ya utumwa.[#Kut 20:2; Law 26:1; Kum 6:4; Zab 81:10]
7Usiwe na miungu mingine ila mimi.[#Kut 20:3]
8Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani, au kilicho majini chini ya nchi.[#Law 26:1; Kum 4:15-18; 27:15; Kut 20:4; Zab 97:7; Mdo 17:29]
9Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,[#Kut 34:6-7; Hes 14:18; Kum 7:9-10]
10nami nawarehemu maelfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.[#Yer 32:18; Dan 9:4; 1 Yoh 1:7]
11Usilitaje bure Jina la BWANA, Mungu wako; maana BWANA hatamhesabia kuwa hana hatia, mtu alitajaye jina lake bure.[#Law 19:12; Kut 20:7; Yak 5:12; Mt 5:33]
12Ishike siku ya Sabato uitakase, kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru.[#Kut 16:23-30; 31:12-14; Kut 20:8; Neh 10:28-29]
13Siku sita fanya kazi, utende mambo yako yote;[#Kut 23:12; 31:15; 34:21; 35:2; Law 23:3; Eze 20:12]
14lakini siku ya saba ni Sabato ya BWANA, Mungu wako; siku hiyo usifanye kazi yoyote, wewe, wala mwanao, wala binti yako, wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala ng'ombe wako, wala punda wako, wala mnyama wako yeyote, wala mgeni aliye ndani ya malango yako, ili mtumwa wako na mjakazi wako wapumzike vile vile kama wewe.[#Mwa 2:2; Kut 16:29; Ebr 4:4]
15Nawe utakumbuka ya kuwa wewe ulikuwa mtumwa katika nchi ya Misri, na ya kuwa BWANA, Mungu wako, alikutoa huko kwa mkono wenye nguvu, na mkono ulionyoshwa; kwa sababu hiyo BWANA, Mungu wako, alikuamuru uishike sabato.
16Waheshimu baba yako na mama yako; kama BWANA, Mungu wako, alivyokuamuru, siku zako zipate kuzidi, nawe upate kufanikiwa katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.[#Kum 27:16; Mt 15:4; 19:19; Mk 7:10; 10:19; Lk 18:20; Efe 6:2,3; Law 19:3; Kol 3:20; Kum 4:40]
17Usiue.[#Mwa 9:6; Law 24:17; Mt 5:21; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11]
18Wala usizini.[#Law 20:10; Mt 5:27; 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9; Yak 2:11]
19Wala usiibe.[#Law 19:11; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; Rum 13:9]
20Wala usimshuhudie jirani yako uongo.[#Kut 23:1; Mt 19:18; Mk 10:19; Lk 18:20; 1 Fal 21:10]
21Wala usimtamani mke wa jirani yako; wala usiitamani nyumba ya jirani yako, wala shamba lake, wala mtumwa wake, wala mjakazi wake, wala ng'ombe wake, wala punda wake, wala kitu chochote alicho nacho jirani yako.[#Rum 7:7; 13:9; Mik 2:2; Hab 2:9; Lk 12:15; Gal 5:14]
22Haya ndiyo maneno ambayo BWANA aliwaambia mkutano wenu wote mlimani kwa sauti kuu toka kati ya moto, na wingu, na giza kuu; wala hakuongeza neno. Akayaandika juu ya mbao mbili za mawe, akanipa.[#Ebr 12:18-19; Kut 24:12]
23Ikawa, mlipoisikia sauti ile toka kati ya giza, na wakati uo huo mlima ule ulikuwa ukiwaka moto, basi, mlinikaribia, naam, wakuu wote wa makabila yenu, na wazee wenu,
24mkasema, Tazama, BWANA, Mungu wetu, ametuonesha utukufu wake, na ukuu wake, nasi tunasikia sauti yake toka kati ya moto; mmeona leo ya kuwa Mungu husema na mwanadamu, naye akaishi.
25Sasa basi, mbona tufe? Maana moto huu mkubwa utatuteketeza; tukiisikia tena sauti ya BWANA, Mungu wetu, tutakufa.
26Maana katika watu wote ni nani aliyeisikia sauti ya Mungu aliye hai, akisema toka kati ya moto, kama vile sisi, asife?[#Kum 4:33]
27Nenda karibu wewe, ukasikie yote atakayoyasema BWANA, Mungu wetu; ukatuambie yote atakayokuambia BWANA, Mungu wetu; nasi tutayasikia na kuyatenda.[#Ebr 12:19]
28Naye BWANA akasikia sauti ya maneno yenu mliyoniambia; BWANA akaniambia, Nimesikia sauti ya maneno ya watu hawa waliyokuambia; wamesema vema yote waliyosema.
29Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao sikuzote, wa kunicha, na kushika amri zangu zote sikuzote, wapate kufanikiwa wao na watoto wao milele![#Kum 32:29; Zab 81:13; Isa 48:18; Yer 44:4; Mt 23:37; Lk 19:42; 2 Kor 5:20; 6:1; 7:1; Ebr 12:25; Kum 11:1; Zab 119:1-5; Lk 11:28; Yn 15:14; Ufu 22:14]
30Enda uwaambie, Rudini hemani mwenu.
31Lakini wewe, simama hapa karibu nami, nami nitasema nawe sheria zote, na amri na hukumu, utakazowafunza, wapate kuzifanya katika nchi niwapayo kuimiliki.[#Mal 4:4; Gal 3:19]
32Tunzeni basi, mtende kama mlivyoamriwa na BWANA, Mungu wenu; msikengeuke kwa mkono wa kulia wala wa kushoto.[#Kum 17:20; 28:14; Yos 1:7; 23:6; Mit 4:27]
33Endeni njia yote aliyowaagiza BWANA, Mungu wenu, mpate kuwa hai, na kufanikiwa, mkafanye siku zenu kuwa nyingi katika nchi mtakayoimiliki.[#Kum 10:12; Zab 119:6; Mhu 8:12; Yer 7:23; Lk 1:6; 1 Tim 4:8; Kum 4:40; 12:25,28; 22:7; Efe 6:3]