Esta 10

Esta 10

1Basi mfalme Ahasuero alitoza kodi katika nchi na katika visiwa vya bahari.[#Mwa 10:5; Zab 72:10; Isa 24:15]

2Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika Kitabu cha Kumbukumbu za Wafalme wa Umedi na Uajemi?

3Kwa maana Mordekai Myahudi akiwa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwajali watu wake, na kuiangalia hali njema ya wazawa wao wote.[#Mwa 41:40; 2 Nya 28:7; Neh 2:10; Zab 122:8; Mit 12:20; Isa 26:12]

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya