The chat will start when you send the first message.
1Neno la BWANA likanijia, kusema,
2Mwanadamu, mzabibu una sifa gani kuliko mti mwingine, au tawi la mzabibu lililokuwa kati ya miti ya msituni?[#Zab 80:8; Hos 10:1]
3Je! Mti wake waweza kutwaliwa, ili kufanya kazi yoyote? Watu waweza kufanya chango kwa huo, ili kutundika chombo chochote?
4Tazama, watupwa motoni kuwa kuni moto unapoziteketeza ncha zake zote mbili, nao umeteketea katikati, je! Wafaa kwa kazi yoyote?[#Yn 15:6]
5Tazama, ulipokuwa mzima, haukufaa kwa kazi yoyote; sembuse ukiisha kuliwa na moto, na kuteketea; je! Waweza kufaa kwa kazi yoyote?
6Basi Bwana MUNGU asema hivi; Kama mzabibu kati ya miti ya msituni, niliyoupa moto uwe kuni, ndivyo nitakavyowatoa wakaao Yerusalemu.
7Nami nitaukaza uso wangu juu yao; nao watatoka motoni, lakini moto utawateketeza; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi BWANA, nitakapoukaza uso wangu juu yao.[#Law 17:10; Zab 34:16; Yer 21:10; 48:43,44; Isa 24:18; Amo 5:19; Eze 6:7; 7:4]
8Nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa, kwa sababu wamekosa, asema Bwana MUNGU.