The chat will start when you send the first message.
1Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja.[#Mdo 2:6]
2Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari; wakakaa huko.[#Dan 1:2]
3Wakaambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa.
4Wakasema, Haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote.[#Kum 1:28; Yn 5:44; Lk 1:51]
5BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu.[#Mwa 18:21; Zab 33:13; 53:2]
6BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya.[#Zab 2:1,4]
7Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao.[#Mwa 1:26; 42:23; Kum 28:49; Yer 5:15; Mdo 2:4-11; 1 Kor 14:2,11,23]
8Basi BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji.[#Mwa 10:25-32; Zab 92:9; Mit 19:29; Lk 1:51]
9Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.[#1 Kor 14:23]
10Hivi ndivyo vizazi vya Shemu; Shemu alikuwa mtu wa miaka mia moja akamzaa Arfaksadi miaka miwili baada ya gharika.[#1 Nya 1:17-27]
11Shemu akaishi baada ya kumzaa Arfaksadi miaka mia tano, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
12Arfaksadi akaishi miaka thelathini na mitano, akamzaa Sela.[#Lk 3:35]
13Arfaksadi akaishi baada ya kumzaa Sela miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
14Sela akaishi miaka thelathini, akamzaa Eberi.
15Sela akaishi baada ya kumzaa Eberi miaka mia nne na mitatu, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
16Eberi akaishi miaka thelathini na minne, akamzaa Pelegi.[#1 Nya 1:19]
17Eberi akaishi baada ya kumzaa Pelegi miaka mia nne na thelathini, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
18Pelegi akaishi miaka thelathini, akamzaa Reu.
19Pelegi akaishi baada ya kumzaa Reu miaka mia mbili na tisa, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
20Reu akaishi miaka thelathini na miwili, akamzaa Serugi.
21Reu akaishi baada ya kumzaa Serugi miaka mia mbili na saba, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
22Serugi akaishi miaka thelathini, akamzaa Nahori.
23Serugi akaishi baada ya kumzaa Nahori miaka mia mbili, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
24Nahori akaishi miaka ishirini na tisa, akamzaa Tera.
25Nahori akaishi baada ya kumzaa Tera miaka mia moja na kumi na tisa, akazaa wana, wa kiume na wa kike.
26Tera akaishi miaka sabini, akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani.[#Mwa 12:1; Yos 24:2; 1 Nya 1:26]
27Na hivi ndivyo vizazi vya Tera. Tera akamzaa Abramu, na Nahori, na Harani. Harani akamzaa Lutu.[#Mwa 12:4; 13:10; 14:12; 19:1,29; 2 Pet 2:7]
28Harani akafa kabla ya baba yake Tera katika nchi aliyozaliwa, yaani, katika Uru wa Wakaldayo.
29Abramu na Nahori wakajitwalia wake. Jina la mkewe Abramu aliitwa Sarai, na jina la mkewe Nahori aliitwa Milka, binti Harani, ambaye alikuwa baba wa Milka na wa Iska.[#Mwa 17:15; 22:20]
30Na Sarai alikuwa tasa, hakuwa na mtoto.[#Mwa 16:1]
31Tera akamtwaa Abramu mwanawe, na Lutu mwana wa Harani, mwana wa mwanawe, na Sarai mkwewe, mke wa Abramu mwanawe, wakatoka wote katika Uru wa Wakaldayo, waende nchi ya Kanaani, wakafika mpaka Harani wakakaa huko.[#Neh 9:7; Mdo 7:4; Ebr 11:8; Mwa 10:19]
32Siku za Tera zilikuwa miaka mia mbili na mitano; Tera akafa katika Harani.