The chat will start when you send the first message.
1Ikawa siku za Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, na Kedorlaoma mfalme wa Elamu na Tidali mfalme wa Goimu,[#Mwa 10:10; Isa 11:11]
2walifanya vita na Bera mfalme wa Sodoma na Birsha mfalme wa Gomora, na Shinabu mfalme wa Adma, na Shemeberi mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari.[#Yak 4:1; Kum 29:23; Mwa 19:22]
3Hawa wote wakakutana katika bonde la Sidimu, yaani Bahari ya Chumvi.[#Kum 3:17; Hes 34:12; Yos 3:16; Zab 107:34]
4Miaka kumi na miwili walimtumikia Kedorlaoma, hata mwaka wa kumi na tatu wakaasi.
5Na mwaka wa kumi na nne akaja Kedorlaoma na wafalme waliokuwa pamoja naye, wakawapiga Warefai katika Ashteroth-karnaimu, na Wazuzi katika Hamu, na Waemi katika Shawe-kiryathaimu,
6na Wahori katika mlima wao Seiri, mpaka Elparani iliyo karibu na jangwa.
7Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.[#2 Nya 20:2]
8Mfalme wa Sodoma, na mfalme wa Gomora, na mfalme wa Adma, na mfalme wa Seboimu, na mfalme wa Bela, ndio Soari, wakatoka wakapanga vita panapo bonde la Sidimu;
9wapigane na Kedorlaoma mfalme wa Elamu, na Tidali mfalme wa Goimu, na Amrafeli mfalme wa Shinari, na Arioko mfalme wa Elasari, wafalme wanne juu ya wale watano.
10Na bonde la Sidimu lilikuwa limejaa mashimo ya lami. Nao wafalme wa Sodoma na Gomora wakakimbia, wakaanguka huko, nao waliosalia wakakimbia milimani.[#Mwa 11:3; 19:17,30]
11Wakachukua mali zote za Sodoma na Gomora na vyakula vyao vyote, wakaenda zao.
12Wakamtwaa Lutu, mwana wa nduguye Abramu, aliyekaa huko Sodoma, na mali yake, wakaenda zao.[#Mwa 11:31; 13:12; Yer 2:17,19]
13Mtu mmoja aliyeponyoka akaenda, akampasha habari Abramu Mwebrania; aliyekuwa akikaa karibu na mialoni ya Mamre, yule Mwamori, ndugu ya Eshkoli, na ndugu ya Aneri, na hao walikuwa wamepatana na Abramu.[#Mwa 14:24]
14Abramu aliposikia ya kwamba nduguye amechukuliwa mateka, akawapa silaha vijana wake, waliozaliwa katika nyumba yake, watu mia tatu na kumi na wanane, akawafuata mpaka Dani.[#Mwa 13:8; 17:27; 15:3; Mhu 2:7; Kum 34:1; Amu 18:29; Isa 41:2]
15Akajipanga apigane nao usiku, yeye na watumwa wake, akawapiga, akawafukuza mpaka Hoba, ulioko upande wa kushoto wa Dameski.
16Naye akarudisha mali zote, akamrudisha Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu.[#1 Sam 30:8,18,19]
17Abramu aliporudi kutoka kumpiga Kedorlaoma na wale wafalme waliokuwa pamoja naye, mfalme wa Sodoma akatoka amlaki katika bonde la Shawe, nalo ni Bonde la Mfalme.[#2 Sam 18:18]
18Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana.[#Ebr 7:1-10; Zab 110:4; Mik 6:6; Mdo 16:17; Ebr 7:10-22]
19Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye Juu Sana, Muumba mbingu na nchi.
20Ahimidiwe Mungu Aliye Juu Sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.[#Ebr 7:4]
21Mfalme wa Sodoma akamwambia Abramu, Nipe mimi hao watu, na hizo mali uchukue wewe.
22Abramu akamwambia mfalme wa Sodoma, Nimeinua mkono wangu kwa BWANA, Mungu Aliye Juu sana, Muumba mbingu na nchi,[#Dan 12:7; Ufu 10:5; Zab 24:1; Mt 11:25]
23ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala chochote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu;[#Est 9:15; 2 Kor 11:9-12]
24isipokuwa hivyo walivyokula vijana, na sehemu za watu waliokwenda nami, yaani, Aneri, na Eshkoli, na Mamre; na watwae wao sehemu zao.