The chat will start when you send the first message.
1Ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Abrahamu, akamwambia, Ee Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa.[#Ebr 11:17-19; Yak 1:12-14]
2Akasema, Umchukue mwanao, mwana wako wa pekee, umpendaye, Isaka, ukaende zako mpaka nchi ya Moria, ukamtoe sadaka ya kuteketezwa huko juu ya mlima mmojawapo nitakaokuambia.[#2 Nya 3:1; Yn 3:16]
3Abrahamu akaondoka alfajiri, akatandika punda wake, akachukua vijana wawili pamoja naye, na Isaka mwanawe, akachanja kuni kwa ajili ya hiyo sadaka ya kuteketezwa, akaondoka, akaenda mpaka mahali alipoambiwa na Mungu.[#Ebr 11:17-19]
4Siku ya tatu Abrahamu akainua macho yake, akapaona mahali pakiwa bado ni mbali.
5Abrahamu akawaambia vijana wake, Kaeni ninyi hapa pamoja na punda, na mimi na kijana tutakwenda kule, tukaabudu, na kuwarudia tena.
6Basi Abrahamu akazitwaa kuni za hiyo sadaka, akamtwika Isaka mwanawe; akatwaa moto na kisu mkononi mwake, wakaenda wote wawili pamoja.[#Yn 19:17; 1 Pet 2:24]
7Isaka akasema na Abrahamu baba yake, akinena, Babangu! Naye akasema, Mimi hapa, mwanangu. Akasema, Tazama! Moto upo, na kuni zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa?
8Abrahamu akasema, Mungu atajipatia mwana-kondoo kwa hiyo sadaka, mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja.[#1 Pet 1:19]
9Wakafika mahali pale alipoambiwa na Mungu, Abrahamu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.[#Yak 2:21; Yn 10:17,18; Ebr 11:17]
10Abrahamu akanyosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe.[#Isa 53:6-12]
11Ndipo malaika wa BWANA akamwita kutoka mbinguni, akasema, Abrahamu! Abrahamu! Naye akasema, Mimi hapa.
12Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu, kwa kuwa hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee.[#1 Sam 15:22; Mwa 26:5; Rum 8:32; Yak 2:22]
13Abrahamu akainua macho yake, akaangalia, na tazama, kondoo dume yuko nyuma yake, amenaswa pembe zake katika kichaka. Basi Abrahamu akaenda akamtwaa huyo kondoo, akamtoa awe sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.[#1 Kor 5:7,8]
14Abrahamu akapaita mahali hapo Yehova-yire, kama watu wasemavyo hata leo, Katika mlima wa BWANA itapatikana.[#22:14 maana yake ni BWANA atapata.; #22:14 ‘atatoa’.]
15Malaika wa BWANA akamwita Abrahamu mara ya pili kutoka mbinguni
16akasema, Nimeapa kwa nafsi yangu asema BWANA, kwa kuwa umetenda neno hili, wala hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,[#Ebr 6:13-14; Zab 105:9; Lk 1:73]
17katika kubariki nitakubariki, na katika kuzidisha nitauzidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, na kama mchanga ulioko pwani; na uzao wako utamiliki lango la adui zao;[#Ebr 11:12; Mwa 15:5; Yer 33:22; Mwa 13:16; 24:60; Mik 1:9]
18na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia; kwa sababu umetii sauti yangu.[#Mdo 3:25; Mwa 12:3; 18:18; Gal 3:8,9,16,18; Mwa 22:3,10; 26:5]
19Basi Abrahamu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Abrahamu akakaa huko Beer-sheba.
20Ikawa baada ya mambo hayo, Abrahamu akaambiwa ya kwamba, Tazama, Milka naye amemzalia Nahori ndugu yako wana;[#Mwa 11:29]
21Usi, mzaliwa wa kwanza wake, na Buzi nduguye, na Kemueli, baba wa Aramu;[#Ayu 1:1; 32:2]
22na Kesedi, na Hazo, na Pildashi, na Yidlafu, na Bethueli.
23Bethueli akamzaa Rebeka; hao wanane Milka alimzalia Nahori ndugu wa Abrahamu.[#Mwa 24:15]
24Na suria wake Reuma naye alizaa Teba na Gahamu na Tahashi na Maaka.