The chat will start when you send the first message.
1Yakobo akainua macho yake, akaona, na tazama, Esau anakuja na watu mia nne pamoja naye. Akawagawanyia Lea, na Raheli, na wale vijakazi wawili, wana wao.[#Mwa 32:6]
2Akawaweka hao vijakazi na wana wao mbele, na Lea na wanawe nyuma yao, na Raheli na Yusufu mwisho.
3Akapita mwenyewe mbele yao, akainama mpaka nchi mara saba, hata alipomkaribia ndugu yake.[#Mwa 18:2; 42:6]
4Esau akaja mbio kumlaki, akamkumbatia, na kumwangukia shingoni, akambusu; nao wakalia.[#Mwa 32:28; Mit 16:1; 21:1; Yer 10:23]
5Akainua macho yake, akawaona wale wanawake na watoto, akauliza, Ni nani hawa walio pamoja nawe? Akasema, Ni watoto Mungu aliompa mtumwa wako kwa neema yake.[#Mwa 48:9; Zab 127:3; Isa 8:18]
6Ndipo wale vijakazi, na wana wao, wakakaribia wakainama.
7Lea naye, na wanawe, wakakaribia wakainama. Baadaye Yusufu na Raheli wakakaribia, wakainama.
8Akasema, Kundi hili lote nililokutana nalo, maana yake ni nini? Akasema, Ili kunipatia kibali machoni pa bwana wangu.[#Mwa 32:5,16]
9Esau akasema, Ninayo tele, ndugu yangu, hifadhi uliyo nayo yawe yako.
10Yakobo akasema, Sivyo; nakuomba kama nimekubalika machoni pako tafadhali upokee zawadi yangu mkononi mwangu, Hakika, kuona uso wako ni kama kuuona uso wa Mungu – maana umenipokea kwa kibali kama chake.[#Mwa 43:3; 2 Sam 3:13; 14:24-32; Mt 18:10]
11Tafadhali pokea zawadi yangu iliyoletwa kwako, kwa sababu Mungu amenineemesha, na kwa sababu ninavyo hivi vyote. Akamsihi sana, naye akapokea.[#Amu 1:15; 1 Sam 25:27; 2 Fal 5:15; Flp 4:18; 2 Fal 5:23]
12Kisha Esau akamwambia, Twende zetu, tusafiri, nami nitakutangulia.
13Akamjibu, Bwana wangu anajua ya kuwa watoto ni wachanga, tena kondoo na ng'ombe nilio nao wanyonyesha. Hao wanyama wakiharakishwa siku moja, watakufa wote.
14Tafadhali bwana wangu na apite mbele ya mtumwa wake; nami nitawaongoza polepole kwa kadiri ya mwendo wa wanyama walio mbele yangu, na kwa kadiri ya mwendo wa watoto, hadi nitakapofika kwa bwana wangu huko Seiri.[#Mwa 32:3]
15Esau akasema, Basi nikuachie, baadhi ya watu walio pamoja nami. Akasema, Pana haja gani? Na nione kibali tu machoni pa bwana wangu.[#Rut 2:13]
16Basi Esau akarudi siku ile ile akishika njia yake mpaka Seiri.
17Yakobo akaendelea mpaka Sukothi. Akajijengea nyumba, akawafanyia makundi yake vibanda. Kwa hiyo jina la mahali pale pakaitwa Sukothi.[#Yos 13:27; Amu 8:5]
18Yakobo akaja kwa amani mpaka katika mji wa Shekemu, ulio katika nchi ya Kanaani, alipokuja kutoka Padan-aramu; akapiga kambi mbele ya huo mji.[#Yn 3:23; Mdo 7:16; Yos 24:1]
19Akainunua sehemu ya nchi, alipopiga hema yake, kwa mkono wa wana wa Hamori, baba wa Shekemu, kwa vipande mia moja vya fedha.[#Yos 24:32; Yn 4:5; Mdo 7:16]
20Akajenga huko madhabahu, akaiita, El-elohe-Israeli.[#Mwa 35:7; #33:20 maana yake ni Mungu, Mungu wa Israeli.]