Yeremia 47

Yeremia 47

Hukumu juu ya Wafilisti

1Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, kuhusu Wafilisti, kabla Farao hajashambulia Gaza.[#Sef 2:4-7; Zek 9:5-7; #Isa 14:29-31; Eze 25:15-17; Yoe 3:4-8; Amo 1:6-8; Sef 2:4-7; Zek 9:5-7]

2BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi wataomboleza.[#Isa 8:7; Yer 1:14]

3Kwa sababu ya kishindo cha kukanyaga kwa kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbio mbio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya mngurumo wa magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu;[#Nah 3:2]

4kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.[#Yer 25:22; Yoe 3:4; Amo 1:9,10; 9:7; Mwa 10:14]

5Upaa umeupata Gaza;[#Sef 2:4]

Ashkeloni umenyamazishwa

Mabaki ya bonde lao;

Hata lini utajikatakata?

6Ee upanga wa BWANA,[#Eze 21:3]

Siku ngapi zitapita kabla hujatulia?

Ujitie katika ala yako;

Pumzika, utulie.

7Utawezaje kutulia,[#1 Sam 3:12; Mik 6:9]

Ikiwa BWANA amekupa agizo?

Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani,

Ndipo alipoyaamuru hayo.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya