Yoshua 15

Yoshua 15

Nchi ya Yuda

1Sehemu waliyopewa wana wa Yuda kwa kufuata jamaa zao ilikuwa imefika mpaka wa Edomu, hadi jangwa la Sini upande wa kusini, huko mwisho upande wa kusini.[#Hes 34:3; 33:36]

2Mpaka wao wa kusini ulikuwa kutoka mwisho wa Bahari ya Chumvi, kutoka ile hori ielekeayo kusini;

3nao ukaendelea upande wa kusini wa kukwea kwenda Akrabimu, kisha ukaendelea hadi Sini, kisha ukaenda upande wa kusini wa Kadesh-barnea, kisha ukaendelea karibu na Hesroni, kisha ukafika Adari, na kuzunguka kwendea Karka;

4kisha ukaendelea hadi Azmoni, na kutokea hapo penye kijito cha Misri; na mwisho wa mpaka huo ulikuwa baharini; huu ndio mpaka wenu wa upande wa kusini.[#Hes 34:5; Mwa 15:18; 1 Fal 8:65]

5Na mpaka wa upande wa mashariki ulikuwa Bahari ya Chumvi, hadi mwisho wa mto wa Yordani. Na mpaka wa upande wa kaskazini ulikuwa kutoka pale penye hori ya baharini mwisho wa mto wa Yordani;

6na huo mpaka ukaendelea hadi Beth-hogla, kisha ukaendelea upande wa kaskazini wa Beth-araba; kisha mpaka ukaendelea hadi jiwe la Bohani mwana wa Reubeni;[#Yos 18:17]

7kisha mpaka ukaendelea hadi Debiri kutoka bonde la Akori, na ukaendelea upande wa kaskazini, kwa kuelekea Gilgali, iliyo mkabala wa kukwelea kwenda Adumimu, ulio upande wa kusini wa mto; kisha huo mpaka ukaendelea hadi kufika kwenye maji ya Enshemeshi, na kuishia Enrogeli;[#Yos 7:26; Isa 65:10; Hos 2:15; 2 Sam 17:17]

8kisha mpaka ukaendelea karibu na bonde la mwana wa Hinomu, na kufika ubavuni mwa huyu Myebusi upande wa kusini (ndio Yerusalemu); kisha mpaka ukaendelea hata kilele cha mlima ulio pale mkabala wa bonde la Hinomu upande wa magharibi, lililo pale mwisho wa bonde la Warefai upande wa kaskazini;[#Yos 18:16,28; 2 Fal 23:10; Yer 19:2,6; Amu 1:21; 19:10; 2 Sam 5:18]

9kisha mpaka ulipigwa kutoka juu ya mlima huo hadi kufika chemchemi ya maji ya Neftoa kisha ukatokea hata miji ya kilima cha Efroni; kisha mpaka ulipigwa hadi kufika Baala (ndio Kiriath-yearimu);[#1 Nya 13:6; Amu 18:12]

10kisha mpaka ukazunguka kutoka Baala kwendelea upande wa magharibi hadi kilima Seiri, kisha ukaendelea hadi upande wa mlima wa Yearimu upande wa kaskazini (huo ndio Kesaloni), kisha ukateremkia Beth-shemeshi, na kwendelea karibu na Timna;[#Mwa 38:13; Amu 14:1]

11kisha mpaka ukaendelea hadi upande wa kaskazini wa Ekroni; tena mpaka ulipigwa hadi Shikroni, na kwendelea mpaka kilima cha Baala, kisha ukatokea hapo Yabneeli; na ukaishia katika bahari.[#Yos 19:43; 1 Sam 5:10]

12Na mpaka wa upande wa magharibi ulifika hadi Bahari Kubwa, na mpaka wake. Huo ndio mpaka wa wana wa Yuda kwa kuzunguka kotekote sawasawa na jamaa zao.[#Hes 34:6; Kum 11:24; Eze 47:20]

Kalebu aichukua milki yake

13Kisha alimpa huyo Kalebu mwana wa Yefune sehemu kati ya wana wa Yuda, kama BWANA alivyomwamuru Yoshua, Kiriath-arba, ndiyo Hebroni (ni huyo Arba aliyekuwa babaye Anaki).[#Yos 14:13; Mwa 23:2; #15:13 Tazama Yoshua 14:15.]

14Huyo Kalebu aliwafukuza watoke hapo hao wana watatu wa Anaki, nao ni Sheshai, na Ahimani, na Talmai, wazawa wa Anaki.[#Amu 1:10; Hes 13:22]

15Kisha akakwea kutoka huko ili kuwaendea wenyeji wa Debiri; jina la Debiri hapo kwanza lilikuwa Kiriath-seferi.[#Yos 10:38]

16Kalebu akasema, Yeyote atakayeupiga Kiriath-seferi na kuutwaa, mimi nitampa Aksa binti yangu awe mkewe.

17Naye Othnieli mwana wa Kenazi, nduguye Kalebu, aliutwaa; basi akampa Aksa binti yake awe mkewe.[#Amu 3:9; Hes 32:12; Yos 14:6]

18Kisha ikawa, hapo huyo mwanamke alipokwenda kwa mumewe, akamtaka aombe shamba kwa baba yake; akashuka katika punda wake; Kalebu akamwuliza, Unataka nikupe nini?[#Amu 1:14; Mwa 24:64; 1 Sam 25:23]

19Huyo mwanamke akasema, Nipe baraka; kwa kuwa umeniweka katika nchi ya kusini, unipe na chemchemi za maji pia. Ndipo akampa chemchemi za maji ya upande wa juu, na chemchemi za maji yaupande wa chini.[#Mwa 33:11]

Miji ya Yuda

20Huu ndio urithi wa kabila la wana wa Yuda sawasawa na jamaa zao.[#Mwa 49:8-12; Kum 33:7]

21Miji ya mwisho ya kabila la wana wa Yuda upande wa kuelekea mpaka wa Edomu katika nchi ya Negebu ilikuwa ni Kabseeli, Ederi, Yaguri;[#Mwa 35:21]

22Kina, Dimona, Adada;

23Kedeshi, Hazori, Ithnani;

24Zifu, Telemu, Bealothi;[#1 Sam 15:4]

25Hazor-hadata, Kerioth-hezroni (ndio Hazori);

26Amamu, Shema, Molada;

27Hasar-gada, Heshmoni, Beth-peleti;

28Hasar-shuali, Beer-sheba, Biziothia;

29Baala, Iyimu, Esemu;

30Eltoladi, Kesili, Horma;

31Siklagi, Madmana, Sansana;[#Yos 19:5; 1 Sam 27:6; 30:1; 1 Nya 12:1]

32Lebaothi, Shilhimu, Aini na Rimoni; miji hiyo yote ni miji ishirini na tisa, pamoja na vijiji vyake.[#Neh 11:29]

33Katika nchi ya Shefela, Eshtaoli, Sora, Ashna,[#Yos 19:41; Hes 13:23]

34Zanoa, Enganimu, Tapua, Enamu;

35Yarmuthi, Adulamu, Soko, Azeka;[#Yos 10:3,5; 12:15; 1 Sam 17:1; Yos 10:10]

36Shaarimu, Adithaimu, Gedera na Gederothaimu miji kumi na minne, pamoja na vijiji vyake.[#1 Sam 17:52]

37Senani, Hadasha, Migdal-gadi;

38Dilani, Mispe, Yoktheeli;[#2 Fal 14:7]

39Lakishi, Bozkathi, Egloni;[#Yos 10:3; 2 Fal 18:14; 19:8; 2 Nya 11:9; 2 Fal 22:1; Yos 12:12]

40Kaboni, Lamasi, Kithilishi;

41Gederothi, Beth-dagoni, Naama na Makeda; miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.

42Libna, Etheri, Ashani;

43Yifta, Ashna, Nesibu;

44Keila, Akizibu na Maresha; miji tisa, pamoja na vijiji vyake.

45Ekroni, pamoja na miji yake na vijiji vyake;

46kutoka huko Ekroni mpaka baharini, yote iliyokuwa upande wa Ashdodi, pamoja na vijiji vyake.[#Yos 13:3; 1 Sam 5:1,6]

47Ashdodi, na miji yake na vijiji vyake; Gaza, na miji yake na vijiji vyake; mpaka kijito cha Misri, na bahari kuu na pwani yake.[#Mwa 15:18; Hes 34:6]

48Na katika nchi ya vilima, Shamiri, Yatiri, Soko;

49Dana, Kiriath-sana (ambao ni Debiri);

50Anabu, Eshtemoa, Animu;

51Gosheni, Holoni na Gilo; miji kumi na mmoja, pamoja na vijiji vyake.[#Yos 10:41; 11:16]

52Arabu, Duma, Eshani;

53Yanumu, Beth-tapua, Afeka;

54Humta, Kiriath-arba (ndio Hebroni) na Siori; miji tisa, pamoja na vijiji vyake.[#Mwa 23:2; Yos 14:15; Amu 1:10]

55Maoni, Karmeli, Zifu, Yuta;

56Yezreeli, Yokdeamu, Zanoa;

57Kaini, Gibea na Timna; miji kumi, pamoja na vijiji vyake.

58Halhuli, Beth-suri, Gedori;

59Maarathi, Bethanothi na Eltekoni; miji sita, pamoja na vijiji vyake.

60Kiriath-baali (ndio Kiriath-yearimu) na Raba; miji miwili, pamoja vijiji vyake.[#Yos 18:14; 1 Sam 7:1,2; 1 Nya 13:6]

61Huko nyikani, Beth-araba, na Midini, na Sekaka;

62na Nibshani, na huo Mji wa Chumvi, na Engedi; miji sita, pamoja na vijiji vyake.[#1 Sam 23:29]

63Tena katika habari ya Wayebusi, hao wenye kukaa Yerusalemu, wana wa Yuda hawakuweza kuwatoa; lakini hao Wayebusi walikaa pamoja na wana wa Yuda huko Yerusalemu hata hivi leo.[#Amu 1:8,21; 19:10-12; Hes 13:29; 2 Sam 5:6; 24:16,18; 1 Nya 11:4; 2 Nya 3:1; Zek 9:7]

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya