The chat will start when you send the first message.
1BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.[#Kut 6:7; Eze 20:5]
3Nanyi msifanye matendo kama yale ya nchi ya Misri mlikokaa; wala msifanye matendo kama yale ya nchi ya Kanaani, nitakayowapeleka; wala msifuate amri zao hao.[#Eze 23:8; Kut 23:24]
4Mtayatii maagizo yangu, na mtazishika amri zangu, ili kuzifuata; mimi ndimi BWANA Mungu wenu.
5Kwa ajili ya hayo mtazishika amri zangu na maagizo yangu yeyote atakayefanya hivyo ataishi; mimi ndimi BWANA.[#Neh 9:29; Eze 18:9; 20:11-13; Lk 10:28; Rum 10:5; Gal 3:12; Isa 44:6; Yer 9:24; Mal 3:6]
6Mtu yeyote miongoni mwenu asimkaribie mwenziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua utupu; mimi ndimi BWANA.
7Utupu wa baba yako, wala utupu wa mama yako, usifunue, maana ndiye mama yako; usifunue utupu wake.
8Utupu wa mke wa baba yako, usifunue; maana, ni utupu wa baba yako.[#Law 20:11; Kum 22:30; 27:20; Mwa 49:4; 1 Kor 5:1]
9Utupu wa dada yako, binti ya baba yako, au binti ya mama yako, awe alizaliwa nyumbani mwenu au kwingine, utupu wa hao usifunue.[#Law 20:17; Kum 27:22; 2 Sam 13:12]
10Utupu wa binti ya mwanao wa kiume, au wa binti ya binti yako, utupu wao hao usifunue; kwa kuwa ni utupu wako mwenyewe.
11Utupu wa binti ya mkewe baba yako, aliyezaliwa na baba yako, yeye ni dada yako, usifunue utupu wake.
12Usifunue utupu wa dada ya baba yako; maana, yeye ni jamaa wa karibu.[#Law 20:19-20]
13Usifunue utupu wa dada ya mama yako; maana, yeye ni jamaa ya mama yako wa karibu.
14Usifunue utupu wa ndugu ya baba yako, usimkaribie mkewe huyo; yeye ni shangazi yako.
15Usifunue utupu wa mkweo mwanamke; yeye ni mke wa mwanao; usifunue utupu wake huyo.[#Law 20:12; Mwa 38:18; Eze 22:11]
16Usifunue utupu wa mke wa nduguyo; maana, ni utupu wa nduguyo.[#Law 20:21; Mt 14:3,4; 22:24]
17Usifunue utupu wa mwanamke na binti yake; usimtwae binti ya mwanaye wa kiume, au binti ya binti yake, ili kufunua utupu wake; hao ni jamaa ya karibu; ni uovu mkuu.[#Law 20:14; Kum 27:23]
18Wala usitwae mwanamke pamoja na dada yake, awe mtesi wake, na kufunua utupu wake, dada yake akiwa hai.[#Mwa 30:15; Mal 2:15; #18:18 Au usimuoe.]
19Usimwendee mwanamke kufunua utupu wake atakapokuwa najisi kwa ajili ya hedhi.[#Law 20:18; Eze 18:6]
20Usilale na mke wa mwenzio, ukajitia unajisi naye.[#Law 20:10; Mit 6:29; Mal 3:5; Mt 5:27,28; 1 Kor 6:9; Ebr 13:4]
21Usimtoe kafara mzawa wako yeyote kwa Moleki na ulinajisi jina la Mungu wako; mimi ndimi BWANA.[#Law 20:1-5; 2 Fal 16:3; Yer 19:5; 1 Fal 11:7,33; Eze 36:20; Mal 1:12; Isa 42:8; #18:21 Moleki ni jina la mungu aliyeabudiwa na Wakanaani, kwa kutoa dhabihu ya watoto wao kwa kuwapitisha motoni. Katika Agano Jipya ni Moloki.]
22Usilale na mwanamume mfano wa kulala na mwanamke; ni machukizo.[#Law 20:13; Rum 1:27; 1 Tim 1:10]
23Wala usilale na mnyama yeyote, ili kujitia unajisi kwake; wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye; ni upotovu.[#Kut 22:18; Law 20:15-16; Kum 27:21]
24Msijitie unajisi katika hata mojawapo ya mambo hayo; kwa maana hayo mataifa nitakayoyatoa mbele zenu yamekuwa najisi kwa mambo hayo yote;[#Mt 15:18; 1 Kor 3:17; Kum 18:12]
25nayo nchi ikawa najisi; na nikaipatiliza kwa ajili ya uovu wake, kisha ikawatema wakazi wake.[#Hes 35:34; Isa 24:5; 26:21; Yer 9:9; 16:18]
26Kwa hiyo mtazishika amri zangu na maagizo yangu, wala msifanye mojawapo ya machukizo hayo; yeye aliye mzaliwa, wala mgeni aishiye kati yenu;
27(kwa kuwa hao watu wa nchi wameyafanya machukizo haya yote, hao waliotangulia mbele zenu, na hiyo nchi imekuwa najisi;)
28ili hiyo nchi isiwatapike na ninyi pia, hapo mtakapoitia unajisi, kama ilivyoitapika hiyo taifa iliyotangulia mbele yenu.
29Kwani mtu yeyote atakayefanya mojawapo ya machukizo hayo, nafsi hizo zitakazoyafanya zitakatiliwa mbali na watu wao.
30Kwa hiyo yafuateni maagizo yangu, ili kamwe msiwe na mojawapo ya tabia hizi zinazochukiza, zilizotangulia kufanywa mbele zenu; mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.