The chat will start when you send the first message.
1Ee Mungu, ukisikie kilio changu,
Uyasikilize maombi yangu.
2Toka mwisho wa nchi nitakulilia ninapozimia moyo,[#1 Tim 2:8]
Uniongoze juu ya mwamba nisioweza kuupanda.
3Kwa maana ulikuwa kimbilio langu,[#Mit 18:10]
Ngome yenye nguvu adui asinipate.
4Nitakaa katika hema yako milele,[#Zab 15:1; 23:6; Ufu 3:12]
Na kupata kimbilio chini ya mbawa zako.
5Maana Wewe, Mungu, umezisikia nadhiri zangu.[#1 Kor 3:21-23]
Umewapa urithi wao waliogopao jina lako.
6Utaziongeza siku za mfalme,
Miaka yake itakuwa kama vizazi vingi.
7Atakaa mbele za Mungu milele,[#Zab 41:12; Lk 1:32]
Ziagize fadhili na kweli zimhifadhi.
8Ndivyo nitakavyoliimbia jina lako daima,[#Zab 56:12]
Ili niondoe nadhiri zangu kila siku.