The chat will start when you send the first message.
1Mungu na atufadhili na kutubariki,[#Zab 4:6; 31:16; 119:135; Hes 6:25,26; 2 Kor 4:6]
Na kutuangazia uso wake.
2Njia yake ijulikane duniani,[#Mdo 13:10; Tit 2:11; Lk 2:30-32]
Wokovu wake katikati ya mataifa yote.
3Watu na wakushukuru, Ee Mungu,[#Isa 24:15,16]
Watu wote na wakushukuru.
4Mataifa na washangilie,[#Zab 96:10]
Naam, waimbe kwa furaha,
Maana kwa haki utawahukumu watu,
Na kuwaongoza mataifa walioko duniani.
5Watu na wakushukuru, Ee Mungu,
Watu wote na wakushukuru.
6Nchi imetoa mazao yake[#Law 26:4; Isa 1:19; Zab 85:9-12]
MUNGU, Mungu wetu, ametubariki.
7Mungu atatubariki sisi;[#Zab 22:27]
Miisho yote ya dunia itamcha Yeye.