The chat will start when you send the first message.
1Kwa hiyo Tobia akamwita Rafaeli, akamwambia,
2Ndugu yangu Azaria, utwae mtumishi mmoja na ngamia wawili, ukaende Rage, mji wa Umedi,
3kwa Gabaeli, ili uniletee ile fedha; tena uje naye kwenye karamu ya arusi. Yaani, Ragueli ameapa nisiondoke mimi.
4Ati! Baba yangu anazihesabu siku, nami nikikawia sana atahuzunika mno.
5Hivyo Rafaeli akaondoka, akaenda akatua kwa Gabaeli, akampa ile hati. Naye akaileta ile mifuko ya fedha yenye mihuri yake, akampa.
6Asubuhi mapema wakaondoka wote wawili wakafika kwenye karamu ya arusi; naye Gabaeli akambariki Tobia na mkewe.