The chat will start when you send the first message.
1Kisha akanionesha Yoshua, kuhani mkuu, amesimama mbele ya malaika wa BWANA, na Shetani amesimama mkono wake wa kulia ili kushindana naye.[#Hag 1:1; Ayu 1:6; Ezr 5:2; Ufu 12:10]
2BWANA akamwambia Shetani, BWANA na akukemee Ewe Shetani; naam, BWANA, aliyechagua Yerusalemu, na akukemee; je, Hiki si kinga kilichotolewa motoni?[#Zab 109:31; Mt 4:10; Lk 22:31; Yud 1:9; Rum 16:20; 8:33; 11:5]
3Basi, Yoshua alikuwa amevaa nguo chafu sana, naye alikuwa akisimama mbele ya malaika.[#Isa 64:6]
4Naye malaika akajibu, akawaambia wale waliosimama mbele yake, akisema, Mvueni nguo hizi chafu. Kisha akamwambia yeye, Tazama, nimekuondolea uovu wako, nami nitakuvika mavazi ya thamani kubwa.[#Ufu 19:8]
5Nikasema, Na wampige kilemba kizuri kichwani pake. Basi, wakampiga kilemba kizuri kichwani pake, wakamvika mavazi; naye malaika wa BWANA akasimama karibu.[#Kut 29:6]
6Kisha malaika wa BWANA akamshuhudia Yoshua, akisema,
7BWANA wa majeshi asema hivi, Ikiwa utaenda katika njia zangu, na kushika maagizo yangu, basi utaihukumu nyumba yangu, na kuzilinda nyua zangu, nami nitakupa haki ya kunikaribia kati yao wasimamao karibu.[#Kum 17:9]
8Sikiliza sasa, Ee Yoshua, kuhani mkuu, wewe na wenzako wanaoketi mbele yako; maana hao ni watu walio ishara ya mambo yajayo; kwa maana, tazama, ninamleta mtumishi wangu, aitwaye Chipukizi.[#Isa 42:1; 4:2; Yer 23:5; 33:15; Zek 6:12]
9Maana, litazame jiwe hili nililoliweka mbele ya Yoshua; katika jiwe moja ziko nyuso saba; tazama, nitachonga maandishi yake, asema BWANA wa majeshi, nami nitauondoa uovu wa nchi hii katika siku moja.[#Isa 28:16; 53:4; Ufu 5:6]
10Katika siku ile, asema BWANA wa majeshi, ninyi mtamwalika kila mtu jirani yake chini ya mzabibu, na chini ya mtini.[#1 Fal 4:25; Mik 4:4]