The chat will start when you send the first message.
1Na wana wa Isakari; Tola, na Puva, na Yashubu, na Shimroni, wanne.[#Mwa 30:17,18; 46:13; Hes 26:23]
2Na wana wa Tola; Uzi, na Refaya, na Yerieli, na Yamai, na Ibsamu, na Shemueli, wakuu wa mbari za baba zao, yaani, wa Tola; watu hodari wa vita katika vizazi vyao; hesabu yao katika siku za Daudi ilikuwa watu ishirini na mbili elfu na mia sita.[#2 Sam 24:1,2; 1 Nya 21:1-5; 27:1]
3Na wana wa Uzi; Izrahia; na wana wa Izrahia; Mikaeli, na Obadia, na Yoeli, na Ishia, watano; wote wakuu.[#1 Nya 5:24]
4Na pamoja nao, katika vizazi vyao, sawasawa na mbari za baba zao, walikuwapo vikosi vya jeshi la vita, watu thelathini na sita elfu; kwa kuwa wake zao na watoto wao walikuwa wengi.
5Na ndugu zao katika jamaa zote za Isakari, watu hodari wa vita, wakihesabiwa kwa vizazi vyao, walikuwa watu themanini na saba elfu.
6Wana wa Benyamini; Bela, na Bekeri, na Yediaeli, watatu.[#Mwa 46:21; Hes 26:38; 1 Nya 8:1]
7Na wana wa Bela; Esboni, na Uzi, na Uzieli, na Yerimothi, na Iri, watano; wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita; nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao watu ishirini na mbili elfu na thelathini na wanne.
8Na wana wa Bekeri; Zemira, na Yoashi, na Eliezeri, na Elioenai, na Omri, na Yeremothi, na Abiya, na Anathothi, na Alemethi. Hao wote ndio wana wa Bekeri.
9Nao wakahesabiwa kwa vizazi vyao, katika vizazi vyao, wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, jumla yao watu ishirini elfu na mia mbili.
10Na wana wa Yediaeli; Bilhani; na wana wa Bilhani; Yeushi, na Benyamini, na Ehudi, na Kenaana, na Zethani, na Tarshishi, na Ahishahari.
11Hao wote ndio wana wa Yediaeli, sawasawa na wakuu wa mbari za baba zao, watu hodari wa vita, kumi na saba elfu na mia mbili, wawezao kwenda vitani katika jeshi.
12Tena Shupimu, na Hupimu, wana wa Iri; na Hushimu, wana wa Aheri.[#Hes 26:38,39]
13Wana wa Naftali; Yaseeli, na Guni, na Yeseri, na Shilemu; wana wa Bilha.[#Mwa 46:24]
14Wana wa Manase; Asrieli, ambaye suria yake, Mwarami, alimzalia, akamzalia na Makiri babaye Gileadi;[#Hes 27:1]
15naye Makiri akatwaa mke kwa Hupimu na Shupimu, ambao umbu lao aliitwa Maaka; na wa pili akaitwa jina lake Selofehadi; na Selofehadi alikuwa na binti.[#Hes 27:1-11]
16Na Maaka mkewe Makiri, akamzalia mwana, akamwita jina lake Pereshi; na jina la nduguye aliitwa Shereshi; na wanawe walikuwa Ulamu, na Rakemu.
17Na wana wa Ulamu; Bedani. Hao ndio wana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase.[#1 Sam 12:11]
18Na umbu lake, Hamolekethi, akamzaa Ish-hodu, na Abiezeri, na Mala.
19Na wana wa Shemida walikuwa Ahiani, na Shekemu, na Liki, na Aniamu.
20Na wana wa Efraimu; Shuthela, na mwanawe huyo ni Beredi, na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Ekada, na mwanawe huyo ni Tahathi;[#Mwa 41:52; 48:14-20; Hes 26:35,36; Kum 33:13,17; Zab 60:7; 108:8]
21na mwanawe huyo ni Zabadi, na mwanawe huyo ni Shuthela; na Ezeri na Ekadi, ambao watu wa Gathi, wenyeji wa nchi, waliwaua, kwa sababu walishuka ili kuzipokonya ng’ombe zao.
22Na Efraimu, baba yao, akaomboleza siku nyingi, wakaja nduguze ili kumfariji.[#Mwa 37:34,35; Yos 7:6; 2 Sam 1:11; 3:31; Ayu 2:11; Zab 69:11; Yoe 2:13; Yn 11:19]
23Naye akamwingilia mkewe, naye akachukua mimba na kuzaa mwana, akamwita jina lake Beria, kwa sababu mna mabaya nyumbani mwake.[#Mwa 35:18; 1 Sam 4:21; 1 Nya 4:9]
24Na binti yake alikuwa Sheera, ambaye alijenga Beth-horoni, wa chini na wa juu, na Uzen-sheera.[#Yos 16:3; 1 Sam 13:18; 2 Nya 8:5]
25Mwanawe ni Refa, na Reshefu, na mwanawe huyo ni Tela, na mwanawe huyo ni Tahani;
26na mwanawe huyo ni Ladani, na mwanawe huyo ni Amihudi, na mwanawe huyo ni Elishama;
27na mwanawe huyo ni Nuni, na mwanawe huyo ni Yoshua.[#Hes 13:8,16]
28Na hizi ndizo hozi zao na makao yao; Betheli na vijiji vyake, na upande wa mashariki Naara, na upande wa magharibi Gezeri na vijiji vyake; na Shekemu pia na vijiji vyake, hata Aza na vijiji vyake;
29na mipakani mwa wana wa Manase; Beth-sheani na vijiji vyake; na Taanaki na vijiji vyake; na Megido na vijiji vyake; na Dori na vijiji vyake. Katika miji hiyo walikaa wana wa Yusufu, mwana wa Israeli.[#Yos 17:7,11; 1 Fal 9:15; Amu 1:22-29]
30Wana wa Asheri; Imna, na Ishva, na Ishvi, na Beria, na umbu lao, Sera.[#Mwa 46:17; 49:20; Hes 26:44,46; Kum 33:24]
31Na wana wa Beria; Heberi, na Malkieli, aliyekuwa babaye Birzaithi.
32Na Heberi akamzaa Yafleti, na Shomeri, na Hothamu, na umbu lao, Shua.
33Na wana wa Yafleti; Pasaki, na Bimhali, na Ashvathi. Hao ndio wana wa Yafleti.
34Na wana wa Shomeri; Ahi, na Roga, na Yehuba, na Aramu.
35Na wana wa nduguye Helemu; Sofa, na Imna, na Sheleshi, na Amali.
36Wana wa Sofa; Sua, na Harneferi, na Shuali, na Beri, na Imra;
37na Bezeri, na Hodu, na Shama, na Shilsha, na Ithrani, na Beera.
38Na wana wa Yetheri; Yefune, na Pispa, na Ara.
39Na wana wa Ula; Ara, na Hanieli na Risia.
40Hao wote ndio wana wa Asheri, wakuu wa mbari za baba zao, watu wateule, hodari wa vita, wakuu wa mashehe. Na hesabu yao waliojumlishwa kwa vizazi vyao kwenda vitani walikuwa watu ishirini na sita elfu.[#Kum 2:14]