3 Yoh 1

3 Yoh 1

Salamu

1Mzee, kwa Gayo mpenzi, nimpendaye katika kweli.[#Mdo 19:29; Rum 16:23; 1 Kor 1:14; 2 Yoh 1:1]

Gayo Apongezwa kwa Ukarimu wake

2Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo.[#2 Yoh 1:4]

3Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, kama uendavyo katika kweli.

4Sina furaha iliyo kuu kuliko hii, kusikia ya kwamba watoto wangu wanakwenda katika kweli.

5Mpenzi, kazi ile ni ya uaminifu uwatendeayo hao ndugu na hao wageni nao,

6waliokushuhudia upendo wako mbele ya kanisa; utafanya vizuri ukiwasafirisha kama ipasavyo kwa Mungu.[#Tit 3:13]

7Kwa maana, kwa ajili ya Jina hilo, walitoka, wasipokee kitu kwa Mataifa.[#Mdo 20:35; 1 Kor 9:12,15]

8Basi imetupasa sisi kuwakaribisha watu kama hao, ili tuwe watenda kazi pamoja na kweli.[#Ebr 13:2; 2 Yoh 1:10]

Diotrefe na Demetrio

9Naliliandikia kanisa neno, lakini Diotrefe, apendaye kuwa wa kwanza kati yao, hatukubali.

10Kwa hiyo, nikija, nitayakumbuka matendo yake atendayo, atoavyo upuzi juu yetu kwa maneno maovu; wala hatoshwi na hayo, ila yeye mwenyewe hawakaribishi hao ndugu, na wale watakao kuwakaribisha, huwazuia, na kuwatoa katika kanisa.

Salamu za Mwisho

11Mpenzi, usiuige ubaya, bali uige wema. Yeye atendaye mema ni wa Mungu, bali yeye atendaye mabaya hakumwona Mungu.[#1 Yoh 3:6,9]

12Demetrio ameshuhudiwa na watu wote, tena na ile kweli yenyewe. Nasi pia twashuhudia, nawe wajua ya kwamba ushuhuda wetu ni kweli.[#Yn 19:35; 21:24]

13Nalikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu.[#2 Yoh 1:12]

14Lakini nataraji kukuona karibu, nasi tutasema uso kwa uso.

15Amani kwako. Rafiki zetu wakusalimu. Wasalimu hao rafiki zetu, kila mtu kwa jina lake.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania