The chat will start when you send the first message.
1Maneno ya Mhubiri, mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu[#1:1 Kiebrania ni Koheleth, yaani, Mhubiri, au Mshauri.]
2Mhubiri asema, Ubatili mtupu, ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili.[#Zab 39:5; 62:9,10; Mhu 4:4-6; Rum 8:20]
3Mtu ana faida gani ya kazi yake yote aifanyayo chini ya jua?[#Mhu 3:9]
4Kizazi huenda, kizazi huja; nayo dunia hudumu daima.[#Zab 104:5; 2 Pet 3:10]
5Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake.[#Zab 19:5]
6Upepo huvuma kusi, hugeuka kuwa kaskazi; hugeuka daima katika mwendo wake, na upepo huyarudia mazunguko yake.[#Yn 3:8]
7Mito yote huingia baharini, walakini bahari haijai; huko iendako mito, ndiko irudiko tena.[#Ayu 38:10; Zab 104:8]
8Mambo yote yamejaa uchovu usioneneka, jicho halishibi kuona, wala sikio halikinai kusikia.[#Mhu 3:1; Mit 27:20]
9Yaliyokuwako ndiyo yatakayokuwako; na yaliyotendeka ndiyo yatakayotendeka; wala jambo jipya hakuna chini ya jua.[#Mwa 8:22; Mhu 3:15]
10Je! Kuna jambo lo lote ambalo watu husema juu yake, Tazama, ni jambo jipya? Limekwisha kuwako, tangu zamani za kale zilizokuwa kabla yetu sisi.
11Hakuna kumbukumbu lo lote la vizazi vilivyotangulia; wala hakutakuwa na kumbukumbu lo lote la vizazi vitakavyokuja, miongoni mwao wale watakaofuata baadaye.
12Mimi, Mhubiri, nalikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu.
13Nikatia moyo wangu ili kuyatafuta yote yanayotendeka chini ya mbingu, na kuyavumbua kwa hekima; ni taabu kubwa ambayo Mungu amewapa wanadamu, ili kutaabika ndani yake.[#Mwa 3:19; Mhu 3:10]
14Nimeziona kazi zote zifanywazo chini ya jua; na, tazama, mambo yote ni ubatili na kujilisha upepo.
15Yaliyopotoka hayawezi kunyoshwa,[#Mhu 7:13]
Wala yasiyokuwapo hayahesabiki.
16Nikatafakari nikisema, Nimejipatia hekima nyingi kupita wote walionitangulia katika Yerusalemu; naam, moyo wangu umeona kwa wingi hekima na maarifa.[#1 Fal 4:29-31; 3:12; Mhu 2:9]
17Nikatia moyo wangu ili kuijua hekima, na kujua wazimu na upumbavu; nikatambua ya kwamba hayo yote nayo ni kujilisha upepo.[#Mhu 2:3; 1 The 5:21]
18Yaani,[#Ayu 28:28; Mhu 7:16; 1 Kor 1:20]
Katika wingi wa hekima mna wingi wa huzuni;
Naye aongezaye maarifa huongeza masikitiko.