Ezr 5

Ezr 5

Ujenzi wa Hekalu Waanza tena

1Basi manabii, Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido, wakawafanyia unabii Wayahudi waliokuwako Yerusalemu na Yuda; waliwafanyia unabii kwa jina la Mungu wa Israeli.[#Hag 1:1; Zek 1:1]

2Ndipo akaondoka Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, wakaanza kuijenga nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na pamoja nao walikuwa manabii wa Mungu, wakiwasaidia.[#Hag 1:12-15; Ezr 6:14; Mhu 12:11; Hag 2:4-9]

3Wakati ule ule Tatenai, liwali wa ng’ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzi wao, wakawajia, wakawaambia, Ni nani aliyewapa amri kuijenga nyumba hii, na kuumaliza ukuta huu?[#Ezr 6:6]

4Ndipo wakawauliza hivi, Majina ya watu wanaofanya ujenzi huu ni nani na nani?

5Lakini jicho la Mungu lilikuwa likiwaelekea wazee wa Wayahudi, hao wasiwazuie, hata habari ile imfikilie Dario, ndipo jawabu litakapopatikana kwa waraka.[#2 Nya 16:9; Ezr 7:6,28; Zab 33:18; Isa 41:10; 1 Pet 3:12]

6Hii ndiyo nakala ya waraka waliyompelekea mfalme Dario; na Tatenai, liwali wa ng’ambo ya Mto, na Shethar-Bozenai, na wenzake wa Kiajemi, waliokuwako huko ng’ambo ya Mto,[#Ezr 4:9]

7walimpelekea waraka nao; na maneno haya yakaandikwa ndani yake;

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania