The chat will start when you send the first message.
1Haya basi, enyi matajiri! Lieni, mkapige yowe kwa sababu ya mashaka yenu yanayowajia.[#Lk 6:24]
2Mali zenu zimeoza, na mavazi yenu yameliwa na nondo.[#Mt 6:19]
3Dhahabu yenu na fedha yenu zimeingia kutu, na kutu yake itawashuhudia, nayo itakula miili yenu kama moto. Mmejiwekea akiba katika siku za mwisho.[#Mit 16:27]
4Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliouzuia kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.[#Kum 24:14-15; Law 19:13; Mal 3:5; Isa 5:9; Ayu 31:38-40]
5Mmefanya anasa katika dunia, na kujifurahisha kwa tamaa; mmejilisha mioyo yenu kama siku ya machinjo.[#Lk 16:19,25; Yer 12:3]
6Mmehukumu mwenye haki mkamwua; wala hashindani nanyi.
7Kwa hiyo ndugu, vumilieni, hata kuja kwake Bwana. Tazama, mkulima hungoja mazao ya nchi yaliyo ya thamani, huvumilia kwa ajili yake hata yatakapopata mvua ya kwanza na ya mwisho.[#Kum 11:14; Yoe 2:23; Zek 10:1; Yer 5:24; Lk 21:19; Ebr 10:36]
8Nanyi vumilieni, mthibitishe mioyo yenu, kwa maana kuja kwake Bwana kunakaribia.[#Ebr 10:25; 1 The 2:16; 3:13]
9Ndugu, msinung’unikiane, msije mkahukumiwa. Angalieni, mwamuzi amesimama mbele ya milango.
10Ndugu, watwaeni manabii walionena kwa jina la Bwana, wawe mfano wa kustahimili mabaya, na wa uvumilivu.[#Mt 5:12]
11Angalieni, twawaita heri wao waliosubiri. Mmesikia habari ya subira yake Ayubu, mmeuona mwisho wa Bwana ya kwamba Bwana ni mwingi wa rehema, mwenye huruma.[#Ayu 1:21-22; 2:10; Zab 103:8; 111:4; Dan 12:12]
12Lakini zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, wala kwa mbingu wala kwa nchi; wala kwa kiapo kinginecho chote; bali ndiyo yenu na iwe ndiyo, na siyo yenu iwe siyo, msije mkaangukia hukumu.[#Mt 5:34-37]
13Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.[#Zab 50:15; Kol 3:16]
14Mtu wa kwenu amekuwa hawezi? Na awaite wazee wa kanisa; nao wamwombee, na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana.[#Mk 6:13]
15Na kule kuomba kwa imani kutamwokoa mgonjwa yule, na Bwana atamwinua; hata ikiwa amefanya dhambi, atasamehewa.[#Mk 16:18]
16Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
17Eliya alikuwa mwanadamu mwenye tabia moja na sisi, akaomba kwa bidii mvua isinyeshe, na mvua haikunyesha juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita.[#1 Fal 17:1; 18:1; Lk 4:25; Mdo 14:15]
18Akaomba tena, mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.[#1 Fal 18:42-45]
19Ndugu zangu, ikiwa mtu wa kwenu amepotelea mbali na kweli, na mtu mwingine akamrejeza;[#Gal 6:1]
20jueni ya kuwa yeye amrejezaye mwenye dhambi hata atoke katika njia ya upotevu, ataokoa roho na mauti, na kufunika wingi wa dhambi.[#Mit 10:12; 1 Pet 4:8; Zab 51:13]