The chat will start when you send the first message.
1Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi.[#Mk 1:12,13; Lk 4:1-13; #Ebr 2:18; 4:15]
2Akafunga siku arobaini mchana na usiku, mwisho akaona njaa.[#Kut 34:28; 1 Fal 19:8]
3Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.[#Mwa 3:1-7]
4Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.[#Kum 8:3]
5Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mji mtakatifu, akamweka juu ya kinara cha hekalu,[#Mt 27:53]
6akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa maana imeandikwa,[#Zab 91:11-12]
Atakuagizia malaika zake;
Na mikononi mwao watakuchukua;
Usije ukajikwaa mguu wako katika jiwe.
7Yesu akamwambia, Tena imeandikwa, Usimjaribu Bwana Mungu wako.[#Kum 6:16]
8Kisha Ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno, akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake,
9akamwambia, Haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.
10Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.[#Kum 6:13]
11Kisha Ibilisi akamwacha; na tazama, wakaja malaika wakamtumikia.[#Yn 1:51; Ebr 1:6,14]
12Basi Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, alikwenda zake mpaka Galilaya;[#Mk 1:14,15; Lk 4:14,15; #Mt 14:3; Mk 6:17; Lk 3:19-20]
13akatoka Nazareti, akaja akakaa Kapernaumu, mji ulioko pwani, mipakani mwa Zabuloni na Naftali;[#Yn 2:12]
14ili litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,[#Isa 8:13; 9:1]
15Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali,[#Isa 8:22—9:1]
Njia ya bahari, ng’ambo ya Yordani,
Galilaya ya mataifa,
16Watu wale waliokaa katika giza
Wameona mwanga mkuu,
Nao waliokaa katika nchi na uvuli wa mauti
Mwanga umewazukia.
17Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.[#Mt 3:2]
18Naye alipokuwa akitembea kando ya bahari ya Galilaya, aliona ndugu wawili, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye, wakitupa jarife baharini; kwa maana walikuwa wavuvi.[#Mk 1:16-20; Lk 5:1-11; #Yn 1:40]
19Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.[#Mt 13:47; Eze 47:10]
20Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.[#Mt 19:27]
21Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili, Yakobo wa Zebedayo, na Yohana nduguye, ambao walikuwamo chomboni pamoja na Zebedayo baba yao, wakizitengeneza nyavu zao; akawaita.
22Mara wakakiacha chombo na baba yao, wakamfuata.
23Naye alikuwa akizunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika masinagogi yao, na kuihubiri Habari Njema ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa kila namna katika watu.[#Mt 9:35; Mk 1:39; Lk 4:15,44; Mdo 10:38]
24Na habari zake zikaenea katika Shamu yote; wakamletea wote waliokuwa hawawezi, walioshikwa na maradhi mbalimbali na mateso, wenye pepo, na wenye kifafa, na wenye kupooza; akawaponya.[#Mk 6:55]
25Na makutano mengi wakamfuata, kutoka Galilaya, na Dekapoli, na Yerusalemu, na Uyahudi, na ng’ambo ya Yordani[#Mk 3:7,8; Lk 6:17-19]