Hes 33

Hes 33

Vituo vya Safari ya Waisraeli Wakitoka Misri

1Hizi ndizo safari za wana wa Israeli, hapo walipotoka nchi ya Misri kwa jeshi zao chini ya mkono wa Musa na Haruni.

2Musa akaandika jinsi walivyotoka katika safari zao, kwa amri ya BWANA; na hizi ndizo safari zao kama kutoka kwao kulivyokuwa.

3Wakasafiri kutoka Ramesesi mwezi wa kwanza, siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza; siku ya pili baada ya Pasaka, wana wa Israeli wakatoka kwa mkono wa nguvu mbele ya macho ya Wamisri wote,[#Mwa 47:11; Kut 1:11; 12:37; 12:2; 13:4; Zab 105:38; Isa 52:12; Kut 14:8]

4hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, BWANA aliokuwa amewapiga kati yao; BWANA akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo.[#Kut 12:12; 18:11; Isa 19:1; Sef 2:11; Ufu 12:8]

5Wana wa Israeli wakasafiri kutoka Ramesesi, wakapanga katika Sukothi.[#Kut 12:37]

6Kisha wakasafiri kutoka Sukothi, wakapanga Ethamu, palipo katika mwisho wa nyika.[#Mwa 33:17; Kut 13:20; Yos 13:27; Zab 60:6]

7Wakasafiri kutoka Ethamu, na kurudi nyuma hata Pi-hahirothi palipokabili Baal-sefoni; wakapanga mbele ya Migdoli.[#Kut 13:17,18; 14:2,9]

8Wakasafiri kutoka hapo mbele ya Hahirothi, wakapita katikati ya bahari na kuingia jangwani; kisha wakaenda safari ya siku tatu katika nyika ya Ethamu, wakapanga Mara.[#Kut 14:22; 15:22]

9Wakasafiri kutoka Mara, wakafikilia Elimu; huko Elimu palikuwa na chemchemi za maji kumi na mbili, na mitende sabini; nao wakapanga hapo.

10Wakasafiri kutoka Elimu wakapanga karibu na Bahari ya Shamu.

11Wakasafiri kutoka Bahari ya Shamu, wakapanga katika nyika ya Sini.[#Kut 16:1; 17:1]

12Wakasafiri kutoka nyika ya Sini, wakapanga Dofka.

13Wakasafiri kutoka Dofka, wakapanga Alushi.

14Wakasafiri kutoka Alushi, wakapanga Refidimu, ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa.[#Kut 17:1; 19:2]

15Wakasafiri kutoka Refidimu, wakapanga katika nyika ya Sinai.[#Kut 16:1; 19:1,2]

16Wakasafiri kutoka nyika ya Sinai, wakapanga Kibroth-hataava.[#Hes 11:34; Kum 9:22]

17Wakasafiri kutoka Kibroth-hataava, wakapanga Haserothi.

18Wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga Rithma.[#Hes 12:16; Kum 1:1]

19Wakasafiri kutoka Rithma, wakapanga Rimon-peresi.

20Wakasafiri kutoka Rimon-peresi, wakapanga Libna.[#Kum 1:1]

21Wakasafiri kutoka Libna, wakapanga Risa.

22Wakasafiri kutoka Risa, wakapanga Keheletha.

23Wakasafiri kutoka Keheletha, wakapanga katika mlima wa Sheferi

24Wakasafiri kutoka huo mlima wa Sheferi, wakapanga Harada.

25Wakasafiri kutoka Harada, wakapanga Makelothi.

26Wakasafiri kutoka Makelothi, wakapanga Tahathi.

27Wakasafiri kutoka Tahathi wakapanga Tera.

28Wakasafiri kutoka Tera, wakapanga Mithka.

29Wakasafiri kutoka Mithka, wakapanga Hashmona.

30Wakasafiri kutoka Hashmona, wakapanga Moserothi.[#Kum 10:6]

31Wakasafiri kutoka Moserothi, wakapanga Bene-yakani.

32Wakasafiri kutoka Bene-yakani, wakapanga Hor-hagidgadi.[#Mwa 36:27; Kum 10:6; 1 Nya 1:42]

33Wakasafiri kutoka Hor-hagidgadi, wakapanga Yotbatha.

34Wakasafiri kutoka Yotbatha, wakapanga Abrona.

35Wakasafiri kutoka Abrona, wakapanga Esion-geberi.[#Kum 2:8; 1 Fal 9:26; 22:48]

36Wakasafiri kutoka Esion-geberi, wakapanga katika nyika ya Sini (ni Kadeshi).[#Hes 13:21; 20:1; Kum 32:51; Yos 15:1]

37Wakasafiri kutoka Kadeshi wakapanga katika mlima wa Hori, katika mpaka wa nchi ya Edomu,[#Hes 20:22,23; 21:4; Eze 47:19]

38Haruni akakwea mlima wa Hori, kwa amri ya BWANA, akafa hapo, katika mwaka wa arobaini baada ya wana wa Israeli kutoka katika nchi ya Misri, mwezi wa tano, siku ya kwanza ya mwezi.[#Hes 20:22-28; Kum 10:6; 32:50]

39Naye Haruni alikuwa mtu wa umri wa miaka mia na ishirini na mitatu hapo alipokufa katika mlima wa Hori.

40Ndipo Mkanaani, mfalme wa Aradi, aliyekaa pande za Negebu katika nchi ya Kanaani akasikia habari za kuja kwao wana wa Israeli.[#Hes 21:1; Amu 1:16]

41Nao wakasafiri kutoka mlima wa Hori, wakapanga Salmona.

42Wakasafiri kutoka Salmona, wakapanga Punoni.

43Wakasafiri kutoka Punoni, wakapanga Obothi.

44Wakasafiri kutoka Obothi, wakapanga Iye-abarimu, katika mpaka wa Moabu.

45Wakasafiri kutoka Iye-abarimu, wakapanga Dibon-gadi.[#Hes 32:34]

46Wakasafiri kutoka Dibon-gadi, wakapanga Almon-diblathaimu.[#Yer 48:22; Eze 6:14]

47Wakasafiri kutoka Almon-diblathaimu, wakapanga katika milima ya Abarimu, kukabili Nebo.[#Hes 21:20; Kum 32:49]

48Wakasafiri kutoka hiyo milima ya Abarimu, wakapanga katika nchi tambarare za Moabu, karibu na mto wa Yordani, hapo Yeriko.[#Hes 22:1]

49Wakapanga karibu na Yordani, tangu Beth-yeshimothi hata kufikilia Abel-shitimu katika nchi tambarare za Moabu.

Maagizo ya Kuishinda Kanaani

50Kisha BWANA akanena na Musa hapo katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko, na kumwambia,

51Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Mtakapovuka mto wa Yordani na kuingia nchi ya Kanaani,[#Kum 7:1; 9:1; Yos 3:17]

52ndipo mtakapowafukuza wenyeji wote wa hiyo nchi mbele yenu, nanyi mtayaharibu mawe yao yote yenye kuchorwa sanamu, na kuziharibu sanamu zao zote za kusubu, kuvunja-vunja mahali pao pote palipoinuka;[#Kut 23:24; 34:12-17; Kum 7:2-5,25,26; Yos 11:12; 23:7; Amu 2:2]

53nanyi mtaishika hiyo nchi kuimiliki na kuketi humo; kwa kuwa mimi nimewapa ninyi hiyo nchi ili mwimiliki.[#Zab 24:1; Kum 10:14; Ayu 41:11; Dan 4:35]

54Nanyi mtairithi nchi kwa kufanya kura, kama jamaa zenu zilivyo; hao walio wengi mtawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka utawapa kama kupunguka kwao; mahali po pote kura itakapomwangukia mtu ye yote, mahali hapo ni pake; mtarithi kama kabila za baba zenu zilivyo.[#Hes 26:54-56]

55Lakini kama hamtaki kuwafukuza wenyeji wa nchi watoke mbele yenu; ndipo hao ambao mtakaowasaza watakuwa kama sindano machoni mwenu, na kama miiba ubavuni mwenu, nao watawasumbua katika hiyo nchi ambayo mwakaa.[#Yos 23:13; Zab 106:34; Kut 23:33; Eze 28:24]

56Kisha itakuwa, kama nilivyoazimia kuwatenda wao, ndivyo nitakavyowatenda ninyi.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania