Zab 11

Zab 11

Wimbo wa Kumtumainia Mungu

1BWANA ndiye niliyemkimbilia.

Mbona mnaiambia nafsi yangu,

Kimbia kama ndege mlimani kwenu?

2Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta,

Wanaitia mishale yao katika upote,

Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.

3Kama misingi ikiharibika,

Mwenye haki atafanya nini?

4BWANA yu katika hekalu lake takatifu.[#Hab 2:20; Efe 5:13; Ebr 4:13]

BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni,

Macho yake yanaangalia;

Kope zake zinawajaribu wanadamu.

5BWANA humjaribu mwenye haki;[#Ayu 5:17; Zab 94:12]

Bali nafsi yake humchukia asiye haki,

Na mwenye kupenda udhalimu.

6Awanyeshee wasio haki mitego,

Moto na kiberiti na upepo wa hari,

Na viwe fungu la kikombe chao.

7Kwa kuwa BWANA ndiye mwenye haki,

Apenda matendo ya haki,

Wanyofu wa moyo watamwona uso wake.

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania