The chat will start when you send the first message.
1Neno la BWANA kwa Bwana wangu,[#Zab 45:6; Mt 22:44; Mk 12:36; Lk 20:42-43; 1 Kor 15:25; Mdo 2:34-35; 1 Kor 15:25; Efe 1:20-22; Kol 3:1; Ebr 1:13; 8:1; 10:12-13]
Uketi mkono wangu wa kuume,
Hata niwafanyapo adui zako
Kuwa chini ya miguu yako.
2BWANA atainyosha toka Sayuni
Fimbo ya nguvu zako.
Uwe na enzi kati ya adui zako;
3Watu wako wanajitoa kwa hiari,[#Amu 5:2; Zab 96:9; Mdo 2:41]
Siku ya uwezo wako;
Kwa uzuri wa utakatifu,
Tokea tumbo la asubuhi,
Unao umande wa ujana wako.
4BWANA ameapa,[#Hes 23:19; Zek 6:13; Ebr 5:6; 6:20; 7:17,21]
Wala hataghairi,
Ndiwe kuhani hata milele,
Kwa mfano wa Melkizedeki.
5Bwana yu mkono wako wa kuume;[#Zab 16:8; 2:5; Rum 2:5; Ufu 11:18]
Ataseta wafalme,
Siku ya ghadhabu yake.
6Atahukumu kati ya mataifa,[#Hab 3:13]
Ataijaza nchi mizoga;
Ataseta kichwa katika nchi nyingi.
7Atakunywa maji ya mto njiani;[#Isa 61:1; Yn 3:34; Isa 53:12]
Kwa hiyo atakiinua kichwa chake.