The chat will start when you send the first message.
1Haleluya.[#1 Nya 16:18,34; 2 Nya 5:13; 7:3; Ezr 3:11; Zab 100:5; 106:1; 107:1; 136:1; Yer 33:11]
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2Israeli na aseme sasa,[#Zab 115:9]
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
3Mlango wa Haruni na waseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
4Wamchao BWANA na waseme sasa,
Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
5Katika shida yangu nalimwita BWANA;[#Zab 18:19]
BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.
6BWANA yuko upande wangu, sitaogopa;[#Ebr 13:6]
Mwanadamu atanitenda nini?
7BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu,[#Zab 54:4]
Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wameshindwa.
8Ni heri kumkimbilia BWANA[#Zab 62:8; Isa 2:22; Yer 17:5,7]
Kuliko kuwatumainia wanadamu.
9Ni heri kumkimbilia BWANA.[#Zab 146:3; Isa 30:2,3]
Kuliko kuwatumainia wakuu.
10Mataifa yote walinizunguka;
Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
11Walinizunguka, naam, walinizunguka;[#Zab 88:17]
Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
12Walinizunguka kama nyuki,[#Kum 1:44; Mhu 7:6]
Walizimika kama moto wa miibani;
Kwa jina la BWANA naliwakatilia mbali.
13Ulinisukuma sana ili nianguke;
Lakini BWANA akanisaidia.
14BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu,[#Kut 15:2; Isa 12:2]
Naye amekuwa wokovu wangu.
15Sauti ya furaha na wokovu
Imo hemani mwao wenye haki;
Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.
16Mkono wa kuume wa BWANA umetukuzwa;[#Kut 15:6]
Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu.
17Sitakufa bali nitaishi,[#Zab 6:5; 73:28]
Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.
18BWANA ameniadhibu sana,[#Mit 3:11,12; 1 Kor 11:32]
Lakini hakuniacha nife.
19Nifungulieni malango ya haki,[#Isa 26:2]
Nitaingia na kumshukuru BWANA.
20Lango hili ni la BWANA,[#Zab 24:7; Isa 35:8]
Wenye haki ndio watakaoliingia.
21Nitakushukuru kwa maana umenijibu,
Nawe umekuwa wokovu wangu.
22Jiwe walilolikataa waashi[#Mt 21:42; Mk 12:10; Lk 20:17; Mdo 4:11; Efe 2:20; 1 Pet 2:4,7; #Mt 21:42; Mk 12:10-11]
Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
23Neno hili limetoka kwa BWANA,[#Ayu 5:9]
Nalo ni ajabu machoni petu.
24Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA,[#2 Kor 6:2]
Tutashangilia na kuifurahia.
25Ee BWANA, utuokoe, twakusihi;[#Mt 21:9; Mk 11:9; Yn 12:13]
Ee BWANA, utufanikishe, twakusihi.
26Na abarikiwe yeye ajaye kwa jina la BWANA;[#Zek 4:7; Mt 21:9; 23:39; Mk 11:9; Lk 13:35; 19:38; Yn 12:13]
Tumewabarikia toka nyumbani mwa BWANA.
27BWANA ndiye aliye Mungu,[#Est 8:16; Mik 7:9; Mal 4:2]
Naye ndiye aliyetupa nuru.
Ifungeni dhabihu kwa kamba
Pembeni mwa madhabahu.
28Ndiwe Mungu wangu, nami nitakushukuru,[#Kut 15:2; Isa 25:1]
Ndiwe Mungu wangu, nami nitakutukuza.
29Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema,
Kwa maana fadhili zake ni za milele.