The chat will start when you send the first message.
1Nalifurahi waliponiambia,[#Isa 2:3; Yer 31:6; Zek 8:21]
Na twende nyumbani kwa BWANA.
2Miguu yetu imesimama
Ndani ya malango yako, Ee Yerusalemu.
3Ee Yerusalemu uliyejengwa[#2 Sam 5:9; Efe 2:21]
Kama mji ulioshikamana,
4Huko ndiko walikopanda kabila,[#Kum 16:16; Kut 16:34]
Kabila za BWANA;
Ushuhuda kwa Israeli,
Walishukuru jina la BWANA.
5Maana huko viliwekwa viti vya hukumu,
Viti vya enzi vya mbari ya Daudi.
6Utakieni Yerusalemu amani;[#Isa 62:6; Yer 51:50]
Na wafanikiwe wakupendao;
7Amani na ikae ndani ya kuta zako,
Na kufanikiwa ndani ya majumba yako.
8Kwa ajili ya ndugu zangu na rafiki zangu
Niseme sasa, Amani ikae nawe.
9Kwa ajili ya nyumba ya BWANA, Mungu wetu,
Nikutafutie mema.