The chat will start when you send the first message.
1Tazama, enyi watumishi wa BWANA,[#Law 8:35; 1 Nya 9:33; Zab 130:6; Lk 2:37]
Mhimidini BWANA, nyote pia.
Ninyi mnaosimama usiku
Katika nyumba ya BWANA.
2Painulieni patakatifu mikono yenu,[#Zab 28:2; 1 Tim 2:8]
Na kumhimidi BWANA.
3BWANA akubariki toka Sayuni,[#Zab 124:8; 128:5]
Aliyezifanya mbingu na nchi.