The chat will start when you send the first message.
1Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu;[#Rum 3:10-12; Zab 10:4; Mit 1:7,22; Mwa 6:12]
Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo,
Hakuna atendaye mema.
2Toka mbinguni BWANA aliwachungulia wanadamu,
Aone kama yuko mtu mwenye akili,
Amtafutaye Mungu.
3Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja,
Hakuna atendaye mema,
La! Hata mmoja.
4Je! Wote wafanyao maovu hawajui?
Walao watu wangu kama walavyo mkate,
Hawamwiti BWANA.
5Hapo ndipo walipoingiwa na hofu nyingi,
Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.
6Mnalitia aibu shauri la mtu mnyonge,
Bali BWANA ndiye aliye kimbilio lake.
7Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni!
BWANA awarudishapo wafungwa wa watu wake;
Yakobo atashangilia,
Israeli atafurahi.